• HABARI MPYA

  Friday, July 14, 2017

  KYLE WALKER ATUA MAN CITY KWA PAUNI MILIONI 54

  Kyle Walker akiwa ameshika jezi ya Manchester City baada ya kukamilisha uhamisho wake PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  WASIFU WA WALKER 

  Wasifu wa klabu:
  Sheffield United (2008-09) - Mechi 7
  Northampton (2008)* - Mechi 9
  Tottenham (2009-) - Mechi 228, mabao 4
  Sheffield United (2009-10)* - Mechi 28
  QPR (2010)* - Mechi 20
  Aston Villa (2011)* - Mechi 18, mabao 2
  TOTAL: Mechi 302, mechi 6
  Timu ya Taifa:
  England (2011-) Mechi 27
  KLABU ya Manchester City imekamilisha uhamisho wa beki Kyle Walker kutoka kwa wapinzani wa Ligi Kuu ya England, Tottenham kwa Pauni Milioni 54.
  Beki huyo wa kimataifa wa England amesaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na timu ya Uwanja wa Etihad na atakuwa akilipwa Pauni 130,000 kwa wiki katika kikosi cha kocha Mspaniola, Pep Guardiola.
  Walker anaondoka Spurs baada ya miaka minane ya kufanya kazi nzuri Uwanja wa White Hart Lane akicheza jumla ya mechi 228 – na anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa kwa dau kubwa City katika dirisha hili la usajili, baada ya mshambuliaji Bernardo Silva na kipa Ederson, waliosajili klabu wakitokea Monaco na Benfica.
  Pauni Milioni 54 ni dau la rekodi ya dunia kwa beki, Walker akipiku dau la Pauni Milioni 50, ambazo Paris Saint-Germain ilitoa kumnunu beki Mbrazil, David Luiz kutoka Chelsea mwaka 2014.
  Walker pia anakuwa mchezaji ghali zaidi Muingereza kuwahi kutokea, akiipiku rekodi iliyowekwa na Raheem Sterling aliposajiliwa City pia kutoka Liverpool.
  City sasa ina wachezaji watatu ghali wa England kikosini mwake, mwingine akiwa ni John Stones mbali ya Walker na Sterling. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KYLE WALKER ATUA MAN CITY KWA PAUNI MILIONI 54 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top