• HABARI MPYA

  Friday, July 28, 2017

  KUNA NINI SANCHEZ NA ARSENAL? SASA ANASEMA MGONJWA

  MSHAMBULIAJI wa Arsenal anayetaka kuondoka, Alexis Sanchez amesema anaumwa na kuondoa uwezekano wa kurejea mazoezi kwenye kikosi cha kwanza cha Washika Bunduki hao kama ilivyotarajiwa na kocha Arsene Wenger.
  Mapema Alhamisi, Arsene Wenger alisema mwanasoka huyo wa kimataifa wa Chile, ambaye mustakabali wake Emirates bado haueleweki, angerejea kuungana na wachezaji wenzake mazoezini Jumapili.
  Lakini Sanchez aliyepiga picha akiwa amejifunga skafu akiwa ndani na mbwa wake, ameibua tetesi kwamba atachelewa zaidi baada ya kusema anaumwa.  Pia amejipiga picha akiwa anaonekana amechoka na kuambatanisha maelezo: ‘Naumwa’.

  Nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez ameposti picha hii akiambatanisha na maelezo: 'Naumwa' PICHA ZAIDI GONGA HAPA  
  Sanchez amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa Arsenal na amekuwa akihusishwa na kuondoka Emirates kwa miezi kadhaa.
  Manchester City, Paris Saint-Germain na Juventus ni miongoni mwa klabu ambazo zinamhitaji mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona, ambaye inafahamika yuko tayari kuutupa chini mtutu bunduki.
  Kufuatia kuongezewa muda wa mapumziko baada ya michuano ya Kombe la Mabara la FIFA alipokuwa na timu yake ya taifa ya Chile, Sanchez anatarajiwa kurejea London Colney wikiendi hii kuelekea mechi yao ya Kombe la Emirates na Sevilla.
  “Alexis na (beki Shkodran) Mustafi, mazoezi yao ya kwanza yatakuwa Jumapili, siku tutakayocheza na Sevilla,” amesema Wenger.
  Arsenal watamenyana na Benfica Jumamosi kabla ya kumenyana na Sevilla. Wiki moja baadaye watamenyana na Chelsea katika Ngao ya Jamii, kabla ya kuanza mbio za Ligi Kuu ya England dhidi ya Leicester City Agosti 11. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUNA NINI SANCHEZ NA ARSENAL? SASA ANASEMA MGONJWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top