• HABARI MPYA

  Wednesday, July 12, 2017

  KUMEKUCHA ROBO FAINALI YA MICHUANO YA AFRIKA

  HATUA ya makundi ya michuano ya klabu Afrika, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho imekamilika mwishoni mwa wiki na sasa mashindano hayo yanaingia katika hatua nyingine ya mtoano, ambayo ni Robo Fainali.
  Timu zilizofuzu Robo Fainali katika Ligi ya Mabingwa ni Ahly Tripoli ya Libya, Esperance, Etoile du Sahel za Tunisia, Ferroviario da Beira ya Msumbiji, USM Alger ya Algeria, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Wydad Athletic Club ya Morocco.
  Zilizoingia Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho ni MC Alger ya Algeria, Club Africain, CS Sfaxien za Tunisia, SuperSport United ya Afrika Kusini, Zesco United ya Zambia, FUS Rabat ya Morocco, Recreativo do Libolo ya Angola na TP Mazembe ya DRC.
  Etoile du Sahel ya Tunisia itakutana na Al Ahly Tripoli ya Libya katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

  RATIBA YA ROBO FAINALI
  Ligi ya Mabingwa Afrika 
  Ahly Tripoli (Libya) vs Etoile du Sahel (Tunisia)
  Al Ahly (Misri) vs Esperance (Tunisia)
  Ferroviario da Beira (Msumbiji) vs USM Alger (Algeria)
  Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs Wydad Athletic Club (Morocco)
  (Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Septemba 8 hadi 10 na marudiano kati ya Septemba 15 na 17 mwaka 2017)
  MC Alger ya Algeria itamenyana na Club Africain ya Tunisia katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika  

  RATIBA YA ROBO FAINALI
  Kombe a Shirikisho Afrika
  MC Alger (Algeria) vs Club Africain (Tunisia)
  SuperSport (Afrika Kusini) vs Zesco (Zambia)
  FUS Rabat (Morocco) vs CS Sfaxien (Tunisia)
  Recreativo do Libolo (Angola) vs TP Mazembe (DRC)
  (Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Septemba 8 hadi 10 na marudiano kati ya Septemba 15 na 17 mwaka 2017)
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUMEKUCHA ROBO FAINALI YA MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top