• HABARI MPYA

    Wednesday, July 12, 2017

    KOCHA MROMANIA AREJEA KUANZA KAZI RASMI AZAM

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu Mromania wa Azam FC, Aristica Cioaba, amerejea nchini jana kutoka mapumzikoni nyumbani, tayari kuanza kuiandaa timu hiyo kwa msimu mpya.
    Cioaba alikosekana kwenye ziara ya wiki moja iliyopita nchinio Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Azam nchini humo, Azam FC.
    Baada ya kikosi ch Azam FC kuwasili Dar es Salaam jana usiku kikitokea nchini Rwanda, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja kwa ajili kuondoa uchovu kabla ya kesho Jumatano kuendelea na maandalizi ya msimu mpya 2017-18.
    Kikosi hicho kilikwenda jijini Kigali nchini humo kwa ajili ya kwenda kusherehesha ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo (Azam Rwanda Premier League) walioutwaa Rayon Sports kwa kucheza nao mechi maalumu ya kirafiki walipokuwa wakikabidhiwa taji hilo Jumamosi iliyopita na kupoteza kwa mabao 4-2.
    Mapumziko hayo hayawahusu wachezaji ambao hawakuwemo kwenye safari hiyo, ambao ni mabeki Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, winga Enock Atta Agyei na mshambuliaji Wazir Junior.
    Wachezaji wote waliotoka kwenye safari hiyo watatakiwa kuendelea na mazoezi kesho jioni wakiungana na wenzao chini ya Kocha Cioaba, isipokuwa Mbaraka Yusuph na Shaaban Idd, ambao ni wagonjwa na hivi sasa wakiendelea na matibabu.
    Ni wachezaji watatu tu ambao bado hawajaripoti, ambao ni Waghana Daniel Amoah, mshambuliaji Samuel Afful na kiungo Mcameroon Stephan Kingue, ambao muda wowote kuanzia sasa watajiunga na wenzao.
    Nahodha Msaidizi, Himid Mao ‘Ninja’, kiungo mpya Salmin Hoza, beki wa kushoto Gardiel Michael na winga Joseph Mahundi aliyeongezwa jana, wenyewe hawamo kikosini kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
    Wachezaji hao wapo Stars, inayoendelea na maandalizi kujiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Jumamosi ijayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MROMANIA AREJEA KUANZA KAZI RASMI AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top