• HABARI MPYA

  Friday, July 07, 2017

  KELECHI IHEANACHO AKARIBIA KUTUA LEICESTER CITY

  KLABU ya Leicester City ipo karibuni kabisa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Kelechi Iheanacho kutoka Manchester City, zote za England kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25, lakini dili hilo linaweza kuchukua wiki kadhaa kukamilika.
  Craig Shakespeare anataka kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji na anataka kukamilisha dili hilo kabla ya kwenda ziara ya Hong Kong kuwania taji la Ligi Kuu Asia.
  City imekuwa radhi kumuuza Iheanacho huku Pep Guardiola akikisuka upya kikosi hicho na Mnigeria huyo ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni, atahamia Uwanja wa King Power.

  Mshambuliaji wa Manchester City, Kelechi Iheanacho yuko karibu kuhamia Leicester City PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Shakespeare tayari amewasajili Harry Maguire na Vicente Iborra wote kwa pamoja kwa dau la Pauni Milioni 29 na anataka kutumia fedha zaidi kuboresha kikosi chake.
  Iheanacho amefunga mabao 21 katika mechi 64 tangu ajiunge na City mwaka 2015, lakini amepoteza nafasi kikosi cha kwanza tangu kuwasili kwa mshambuliajin Gabriel Jesus kutioka Brazil.
  Shakespeare anataka kuongeza nguvu mpya kikosini katika safu ya ushambuliaji, lakini yuko tayari kusikiliza ofa za mchezaji aliyesajiliwa kwa dau la rekodi, Islam Slimani.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KELECHI IHEANACHO AKARIBIA KUTUA LEICESTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top