• HABARI MPYA

  Saturday, July 08, 2017

  GHAFLA CHELSEA WAMRUDIA LUKAKU NA DAU SAWA NA LA MAN UNITED

  GHAFLA Chelsea imerudi kwenye kinyang'anyiro cha saini ya mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku baada ya kukubali kutoa ada ya uhamisho sawa na wanayotaka kutoa Manchester United.
  Antonio Conte ameghairi kuachana na mpango wake namba moja wa kumsajili Lukaku na Chelsea pia imekubali vipengele binafasi kama vya timu ya Old Trafford walivyoahidi kwa Mbelgiji huyo.
  Lakini United, ambayo italipa angalau Pauni Milioni 75 kukamilisha dili hilo, inabaki katika nafasi nzuri ya kumpata mchezaji huyo.

  Chelsea imerudi kwenye mbio za kuwania saini ya Romelu Lukaku baada ya kukubali kutoa dau sawa na la Man United PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Chelsea haitalipa kile inachofikiri ada ya uhamisho wa mchezaji huyo tu, bali pia itatakiwa kulipa na Pauni Milioni 12 kwa wakala wa Lukaku, Mino Raiola, ambayo ni silaha muhimu kwa United.
  Awali Lukaku alikuwa kwenye mawasiliano na Conte na kuweka wazi alikuwa anafikiria kurejea katika klabu hiyo iliyomleta England kutoka Anderlecht ya kwao Ubelgiji akiwa kijana mdogo mwaka 2011.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GHAFLA CHELSEA WAMRUDIA LUKAKU NA DAU SAWA NA LA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top