• HABARI MPYA

  Tuesday, July 11, 2017

  CARRICK NDIYE NAHODHA MPYA MANCHESTER UNITED

  Kiungo wa Manchester United, Michael Carrick akitabasamu katika mazoezi ya kwanza kama Nahodha wa timu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  RATIBA YA MECHI ZA MAN UTD KUJIANDAA NA MSIMU MPYA 

  Julai 16 - LA Galaxy - StubHub Center, Los Angeles
  Julai 18 - Real Salt Lake - Uwanja wa Rio Tindo, Utah
  Julai 21 - Manchester City - Uwanja wa NRG, Houston 
  Julai 23 - Real Madrid - Uwanja wa Levi, Santa Clara
  Julai 27 - Barcelona - FedEX Field, Maryland
  Julai 30 - Valerenga - Uwanja wa Ullevaal, Oslo
  Agosti 2 - Sampdoria, Uwanja wa Aviva, Dublin 
  ZIARA YA MAREKANI MAANDISHI MEUSI
  KLABU ya Manchester United imemthibitisha Michael Carrick kuwa Nahodha mpya, baada ya Wayne Rooney kuondoka.
  Rooney ameondoka Manchester kurejea Everton baada ya miaka 13 na sasa Carrick anakuwa Nahodha mpya.
  Kikosi cha Mashetani hao Wekundu kwa sasa kipo mjini Los Angeles, Marekani na nyota wake mbalimbali, akiwemo mshambuliaji mpya, Romelu Lukaku kutoka Everton na kiungo nyota, Paul Pogba kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Nyota hao wa Old Trafford leo wamefanya mazoezi kwenye jua angavu la asubuhi viwanja vya mazodezi vya UCLA katika ziara yao ya Marekani.
  Lukaku alichangamsha mazoezi hayo ya awali akipigwa picha amewabeba wote, Paul Pogba na Jess Lingard uwanjan. Hayo yalikuwa mazoezi ya pili kwa Mbelgiji na wachezaji wenzake wapya, baada ya kusajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 75 kutoka Everton.
  Hata kocha Jose Mourinho akajikuta anatabasamu wakati akiwaagalia nyota wake walivyoanza mazoezi kufuatia mapumziko ya baada ya msimu. Lakini muda mrefu kazi halisi itaanza kwa kuanza na mechi nne wiki ijayo.
  Mashetani hao Wekundu watacheza na LA Galaxy na Real Salt Lake City kabla ya kumenyana na vigogo wenzao wa Ulaya, Manchester City na Real Madrid na kurejea Manchester.
  Kisha watacheza mechi mbili zaidi upande mwingine wa Atlantic, wakimenyana na Valerenga mjini Oslo kabla ya kumaliza na Sampdoria mjini Dublin.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CARRICK NDIYE NAHODHA MPYA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top