• HABARI MPYA

  Friday, July 07, 2017

  AZAM FC YAWASILI SALAMA RWANDA, KUCHEZA NA RAYON KESHO KIGALI

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  KIKOSI cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kimewasili salama jijini Kigali, Rwanda usiku wa kuamkia leo, tayari kabisa kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao Rayon Sports.
  Safari ya kikosi hicho imechukua takribani siku mbili, ambapo itamenyana na mabingwa hao wa Rwanda kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Nyamirambo saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
  Azam FC imefikia katika Hoteli ya Hilltop iliyopo jijini hapa, ambapo kwa mujibu wa programu ya benchi la ufundi, kikosi hicho kitafanya mazoezi leo jioni muda utakaopigwa mchezo huo.
  Rayon Sports itautumia mchezo huo kama sehemu maalumu ya kusheherekea ubingwa wao wa ligi walioutwaa msimu huu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWASILI SALAMA RWANDA, KUCHEZA NA RAYON KESHO KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top