• HABARI MPYA

    Sunday, July 09, 2017

    AZAM FC ‘YACHEZEA’ 4-2 KWA RAYON KIGALI

    Na Mwandishi Wetu, KIGALI
    AZAM FC jana imechapwa mabao 4-2 na Rayon Sport ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu mpya Uwanja wa Amahoro, Kigali.  
    Mabao ya Rayon yalifungwa na Pierre Kwizera dakika ya 30, Nshuti Savio dakika ya 49, Muhire Kevin dakika ya 67 na Shassir Nahimana dakika ya 90 na ushei, wakati ya Azam FC yalifungwa na Yahya Mohamed dakika ya 55 na Mudathir Yahya dakika ya 42.
    Wamepigwa 4-2; Kikosi cha Azam FC kilichoanza jana dhidi ya Rayon 
    Unamkumbuka? Pierre Kwizera ambaye amewahi kuchezea Simba ya Dar es Salaam akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Rayon jana  

    Kocha Iddi Nassor ‘Cheche’ aliyekosa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza ambao bado hawajaripoti kwa sababu mbalimbali, baada ya mchezo alisema uchovu uliwaponza.
    “Nadhani ni uchovu, tumekuja kwa basi na baada ya siku moja tunaingia kwenye mchezo. Wenzetu walikuwa vizuri na walijiandaa kikamilifu matokeo yake wametufunga,”alisema.
    Kikosi cha Rayon kilikuwa; Ndayishimiye Eric Bakame, Manzi Thierry, Mugabo Gabriel, Munezero Fiston, Niyonzima Olivier, Kwizera Olivier, Nova Bayama, Muhire Kevin, Nahimana Shassir, Kakule Mugheni Fabrice na Nshuti Savio Dominique.
    Azam FC; Mwadini Ali/Metecha Mnata dk75, Ismail Gambo/Mohammed Ramadhan dk75, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, David Mwantika, Mudathir Yahya, Abdallah Masoud ‘Cabaye’, Frank Domayo, Yahya Mohammed/Joseph Kimwanga dk58, Yahya Zayed na Iddi Kipagwile.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC ‘YACHEZEA’ 4-2 KWA RAYON KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top