• HABARI MPYA

  Monday, June 05, 2017

  ZESCO YAITANDIKA 1-0 LIBOLO NA KUPANDA KILELENI SHIRIKISHO

  TIMU ya Zesco United jana imepata ushindi wa 1-0 dhidi ya Recreativo Desportivo do Libolo katika mchezo wa Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia.
  Katika mchezo huo, timu zote zilimaliza pungufu, Libolo wakimpoteza Celson Costa na Zesco wakimpoteza Anthony Akum baada ya wote kuonyeshwa kadi za pili za njano na kutilewa kwa kadi nyekundu dakika za 86 na 87.
  Baada ya kuonyeshwa kadi za njano kwa rafu za mapema kwenye mchezo huo, Costa kwa kumchezea rafu Dave Daka kwenye eneo la penalti la Libolo na Akum kwa kumchezea rafu Julsy Kaya na refa wa Namibia, Jackson Pavaza hakusita kuwatoa nje kwa kadi za pili za njano zikiwa zimebaki dakika tatu mchezo kumalizika.
  Bao pekee la washindi lilipatikana dakika ya 26 katika mchezo hup, mfungaji Idriss Mbombo aliyemalizia krosi ya Dave Daka na sasa Zesco United wanaongoza Kundi C baada ya Smouha na El Hilal El Obeid kutoka sare ya 1-1.
  Sasa wana pointi sita baada ya kucheza mechi tatu, wakati Smouha ni ya pili ikiwa na pointi nne ikitofautiana tu kwa wastani wa mabao na El Hilal El Obeid katika nafasi ya tatu na Recreativo Desportivo do Libolo inashika mkia kwa pointi zake tatu.
  Mechi zijazo za kundi hilo zitachezwa Juni 20, wakati Zesco United itakaposafiri kuifuata Clube Recreativo Desportivo do Libolo na El Hilal El Obeid watawakaribisha Smouha.

  MATOKEO YOTE KOMBE LA SHIRIKISHO;
  Juni 4, 2017  
  CS Sfaxien 3 - 0 Platinum Stars
  TP Mazembe 2 - 2 Supersport United
  ZESCO United 1 - 0 Recreativo do Libolo
  Juni 3, 2017
  Smouha SC 1 - 1 Al Hilal Al Ubayyid
  CF Mounana 0 - 1 Horoya
  KCCA 2 - 1 Rivers United FC
  FUS Rabat 2 - 1 Club Africain
  Juni 2, 2017  
  Mbabane Swallows 0 - 0 MC Alger
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZESCO YAITANDIKA 1-0 LIBOLO NA KUPANDA KILELENI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top