• HABARI MPYA

    Tuesday, June 06, 2017

    ZAMU YA SIMBA SC ‘MNYAMA’ SHAMBA LA BIBI LEO

    RATIBA NA MATOKEO SPORTPESA SUPER CUP
    Juni 5, 2017
    Singida United 1-1 AFC Leopards (Penalti 4-5)
    Yanga SC 0-0 Tusker FC (Penalti 4-2)
    Juni 6, 2017
    Jang`ombe Boys vs Gor Mahia
    Simba Vs Nakuru All Star
    NUSU FAINALI
    Juni 8, 2017
    AFC Leopards Vs Yanga SC
    Simba SC/Nakuru All Star Vs Jangombe Boys/Gor Mahia
    FAINALI
    Juni 11, 2017 

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WASHINDI wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba leo wanatupa kete yao ya kwanza kwenye michuano ya SportPesa Super Cup watakapomenyana na Nakuru All Stars Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Mchezo huo utaanza Saa 8:00 mchana na utafuatiwa na mchezo wa pili wa kundi hilo, baina ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya hapo hapo Uhuru.
    Michuano hiyo ilianza jana Uwanja wa Uhuru, mabingwa wa Tanzania wakiwang’oa mabingwa wa Kenya, Tusker FC kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
    Awali ya hapo, vigogo wa Kenya, AFC Leopards nao waliitupa nje Singida United kwa penalty 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 pia.
    Bingwa wa michuano hii atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 30,000 zaidi ya Sh. Milioni 65 za Tanzania pamoja na nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Everton ya England.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMU YA SIMBA SC ‘MNYAMA’ SHAMBA LA BIBI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top