• HABARI MPYA

  Wednesday, June 07, 2017

  VODACOM ‘WATIA MKONO’ SPORTPESA SUPER CUP

  RATIBA NA MATOKEO SPORTPESA SUPER CUP
  Juni 5, 2017
  Singida United 1-1 AFC Leopards (Penalti 4-5)
  Yanga SC 0-0 Tusker FC (Penalti 4-2)
  Juni 6, 2017
  Jang`ombe Boys 0-2 Gor Mahia
  Simba 0-0 Nakuru All Star (Penalti 4-5)
  NUSU FAINALI
  Juni 8, 2017
  AFC Leopards Vs Yanga SC (Saa 8:00 mchana)
  Nakuru All Star Vs Gor Mahia (Saa 10:00 jioni)
  FAINALI
  Juni 11, 2017 
  Na Hussein Mwamba, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imejitokeza kupiga jeki michuano ya SportPesa Super Cup inayoingia kwenye hatua ya Nusu Fainali kesho.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude amesema kwamba wapenzi wa soka nchini watarajie burudani kubwa kutoka kwenye michuano hiyo baada ya kampuni yake kuingia.
  “Kama inavyofahamika Vodacom tumekuwa mstari wa mbele kwenye kudhamini michezo na hususan mpira wa miguu na ninafikiri Watanzania wengi wanafahamu kwamba sisi tumekuwa wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom na hivyo basi baada ya ligi hii kusimama, tukaamua kuungana na wenzetu SportPesa katika kuwaletea buruani wananchi,”amesema.
  Kaude amesema kwamba kwa kushirikiana na waandaaji wa michuano hiyo, kampuni ya SportPesa yenyewe wanatarajiwa kuwapa Watanzania ladha nzuri kama ambayo wamekuwa wakiipata kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 


  Amewataka wapenzi wa soka nchini kutembelea kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ya Vodacom kushiriki promosheni za kujishindia tiketi za kuingia uwanjani kushuhudia mechi zilizobaki kwenye michuano hiyo.
  Timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano hiyo, baada ya Simba, Jang’ombe Boys na Singida United kutolewa, Yanga itamenyana na Leopards katika Nusu Fainali ya kwanza ya michuano ya SportPesa Super Cup kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Nusu Fainali nyingine kesho itazikutanisha timu za Kenya tupu, Gor Mahia iliyoitoa Jang’ombe Boys ya Zanzibar jana kwa mabao 2-0 ya Meddie Kagera na Nakuru All Stars iliyoitoa Simba SC ya Dar es Salaam kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  Vijana wadogo wa Yanga wakiongezewa nguvu na kaka zao wachache tu, akiwemo Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa kikosi cha Yanga, waliwastaajabisha watu juzi baada ya kuwazima mabingwa wa Kenya, Tusker FC kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VODACOM ‘WATIA MKONO’ SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top