• HABARI MPYA

  Wednesday, June 14, 2017

  UFARANSA PUNGUFU YAICHAPA ENGLAND 3-2 KIRAFIKI PARIS

  Kiungo Paul Pogba wa Ufaransa akimiliki mpira ya Kieran Tripper wa England katika mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa Stade de France mjini Paris. Ufaransa walishinda 3-2 pamoja na kumaliza pungufu baada ya Raphael Varane kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika 97 kufuatia refa, Davide Massa kutumia ushahidi wa video baada ya utata uliojitokeza.
  Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Samuel Umtiti dakika ya 22, Djibril Sidibe dakika ya 43 na Ousmane Dembele dakika ya 78, wakati ya England yalifungwa na Harry Kane yote, la kwanza dakika ya tisa akimalizia pasi ya Ryan Bertrand na la pili kwwa penalti dakika ya 48 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA PUNGUFU YAICHAPA ENGLAND 3-2 KIRAFIKI PARIS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top