• HABARI MPYA

  Monday, June 12, 2017

  UCHAGUZI MKUU TFF KUFANYIKA AGOSTI 12 DODOMA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SAALAAM
  UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma, imesema taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo.
  “Napenda kuwatangazia wadau wote wa mpira wa miguu kuwa mnakaribishwa kugombea nafasi zilizo orodheshwa hapo chini kwa kuchukua fomu Ofisi za TFF Karume Ilala na pia unaweza kuzipata katika tovuti ya TFF: www.tff.or.tz,” amesema Kuuli.
  Akitangaza tarehe hiyo mbele ya wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli, amesema kwamba kamati yake haitakuwa na huruma kwa ishara yoyote ya rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi ana nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi ujao kutokana na mafanikio yake katika awamu yake ya kwanza  
  Wakili Kuuli amesema kamati yake itandesha uchaguzi huo kwa Uhuru na Haki na kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zote zilizopo.
  Kuuli, amesema Kamati yake itafanya kazi na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na jeshi la Polisi kuhakikisha uchaguzi huo hautakuwa na vitendo vya rushwa.
  “Tunawatahadharisha wagombea woye kukaa mbali na vitendo vya rushwa…, kamati yetu haitakubali vitendo hivyo na tutafanya kazi na mamlaka za Serikali kuhakikisha yeyote atakayehusika na vitendo hivi anachukuliwa hatua, Takukuru wataufuatilia kwa karibu uchaguzi huu,” alisema Kuuli.
  Akizungumzia mchakato mzima, Kuuli anasema, mchakato wa kuchukua fomu na kuzirejesha ni Juni 16 mpaka 20, mwaka huu na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21 mkapa Juni 23.
  Juni 24 na 25, mwaka huu, kamati itafanya kazi ya kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo majina ya wagombea wakati Juni 26-28 zitakuwa siku za kupokea na kuweka mapingamizi kwa wagombea na Juni 29 mpaka Julai Mosi itakuwa kipindi cha kupitia mapingamizi yote na kufanya usaili.
  Kwa mujibu wa Kuuli, Julai 2-3 kitakuwa kipindi cha kuchapisha na kubandika matokeo ya usaili, Julai 4-7 na kipindi cha Sektretarieti kuwasilisha masuala ya Kimaadili kwenye Kamati ya maadili, Julai 7-11 ni kipindi cha kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya kimaadili.
  Julai 15-17 kitakuwa kipindi cha kukataa Rufaa kwa maamuzi ya  masuala ya kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF, Julai 18-22 itakuwa siku ya kusikiliza rufaa za maadili na Julai 23 mpaka Julai 25 itakuwa siku ya kutoa maamuzi ya Rufaa, Julai 26-28 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa dhidi ya kamati ya Uchaguzi kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, rufaa hizo zitasikilizwa Julai 29 mpaka Agosti 2.
  Wagombea watajulishwa matokeo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Agosti 5-6 itakuwa siku ya kuchapisha majina ya wagombea watakaoingia kwenye Uchaguzi huo na kampeni kwa wagombea zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata yaani Agosti 12 itakuwa siku ya uchaguzi wa viongozi wa TFF.
  Nafasi zinazogombewa ni Rais wa TFF, Makamu wa Rais pamoja na nafasi 13 za wajumbe TFF wanaowakilisha kanda 13 za Kagera na Geita;
  Mara na Mwanza;
  Shinyanga na Simiyu;
  Arusha na Manyara;
  Kigoma na Tabora;
  Katavi na Rukwa;
  Mbeya na Iringa;
  Njombe na Ruvuma;
  Lindi na Mtwara;
  Dodoma na Singida;
  Pwani na Morogoro;
  Kilimanjaro na Tanga na
  Dar es Salaam ambayo ni kanda pekee.
  Sifa za wagombea
  GHARAMA ZA KUCHULIA FOMU.
  1.   Rais TSHS 500,000/=
  2.   Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
  3.   Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/-

  SIFA ZA WAGOMBEA.
   1. 1. Awe raia wa Tanzania.
   2. 2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha   Elimu ya Sekondari).
   3. 3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
   4. 4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
   5. 5. Awe na umri angalau miaka 25.
   6. 6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
   7. 7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
   8. 8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
  Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi (10:00) jioni.

  MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI NI KAMA UFUATAVYO:
  1
  14-15/06/2017

  Kutangaza mchakato wa Uchaguzi wa TFF nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo 
  Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi TFF


  10.7  2
  2
  16-20/06/2017
  Kuanza kuchukua fomu za kugombea. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi.
  Wagombea wote  10.8


  5
  3
  21-23/06/2017

  Kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na Kuandika barua za Kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali
  Kamati ya Uchaguzi TFF

  11.1

  3
  4
  24-25/06/2017

  Kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea
  Kamati ya Uchaguzi TFF

  11.2

  2
  5
  26-28/06/2017

  Kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea
  Wagombea
  11.3 - 4
  3
  6
  29/6-1/7/2017

  Kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa wagombea
  Kamati ya uchaguzi na Wagombea

  11.7

  3
  7
  02-03/07/2017

  Kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo   Matokeo ya awali ya usaili
  Kamati ya Uchaguzi TFF

  11.8

  2
  8
  04-06/07/2017
  Sekretariati kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya Maadili
  Kamati ya maadili ya TFF

  11.10

  3
  9
  07-11/07/2017
  Kipindi cha Kupokea na kusikiliza na kutolea Maamuzi masuala ya maadili
  Kamati ya Maadili ya TFF
  11.10
  5
  10
  12-14/07/2017
  Kutangaza matokeo ya maamuzi ya kamati ya Maadili

  Kamati ya Maadili ya TFF
  11.10
  3
  11
  15-17/07/2017
   Kipindi cha kukata Rufaa kwa Maamuzi ya Masuala ya Kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF
  Wagombea


  11.11

  3
  12
  18-22/07/2017

  Kusikiliza rufaa za kimaadili

  Kamati ya rufaa ya maadili  ya TFF na Wagombea. 

  11.12

  5
  13
  23-25/07/2017
  Kutoa maamuzi ya Rufaa
  Kamati ya rufaa ya maadili  ya TFF.

  11.12
    
  3
  14
  26-28/07/2017
  Kipindi cha Kukata Rufaa Dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF
  Wagombea na Katibu Mkuu TFF.

  13.1

  3
  15
  29/7-2/8/2017
  Rufaa kusikilizwa na kamati ya rufaa ya Uchaguzi ya TFF
  Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF na Wagombea

  13.2

  5
  16
  03-04/08/2017
  Wagombea na kamati ya uchaguzi kujulishwa maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF
  Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF

  13.3-4

  2
  17
  05-06/08/2017
  Kuchapisha orodha ya Mwisho ya Wagombea na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo
  Kamati ya uchaguzi TFF.


  14.1


  2
  18
  07-11/08/2017
  Kipindi cha kampeni kwa wagombea
  Wagombea
  14.3
  5

  19
  12/08/2017
  Uchaguzi Mkuu wa TFF
  Wagombea 
  Wajumbe na Kamati ya Uchaguzi TFF
  14.4
  1
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UCHAGUZI MKUU TFF KUFANYIKA AGOSTI 12 DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top