• HABARI MPYA

    Wednesday, June 14, 2017

    TFF YAMPUUZA KIGANJA, YAENDELEA NA MCHAKATO WAKE WAKE WA UCHAGUZI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limewataka wote wenye nia ya kuwania uongozi wa shirikisho hilo kujitokeza kuchukua fomu kuanzia Juni 16, mwaka huu.
    Tarehe hiyo ni ileile iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli alipozungumza na wanahabari Jumatatu wiki alipotangaza ratiba nzima ya Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
    Taarifa ya TFF imesema kwamba kwa kuwa tovuti ya TFF kwa sasa ipo kwenye marekebisho, zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi TFF litafanyika kwenye ofisi za TFF zilizopo Ilala, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya Juni 16 Saa 10:00 jioni hadi Juni 20, mwaka huu.
    Fedha za kulipia fomu hizo zitalipiwa Benki ya CRDB kupitia namba ya akaunti 01J1019956700 ambako mgombea atawajibika kuwasilisha stakabadhi ya malipo kutoka benki na kupewa fomu ya nafasi husika.
    Gharama za kuchukulia fomu ni Sh. 500,000 kwa nafasi ya Urais, Sh. 300,000 kwa Makamu wa Rais na Sh. 200,000 nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAMPUUZA KIGANJA, YAENDELEA NA MCHAKATO WAKE WAKE WA UCHAGUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top