• HABARI MPYA

  Thursday, June 08, 2017

  STARS NA MAMBA WA LESOTHO KUCHEZWA CHAMAZI USIKU

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kwanza wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji, Tanzania ‘Taifa Stars’ na Lesotho ‘Mamba’ utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi kuanzia Saa 2:00 usiku.
  Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana usiku katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online.
  Na Malinzi amesema sababu za mchezo huo kufanyika Uwanja wa klabu ya Azam ni kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika matengenezo madogo.
  Nahodha Mbwana Samatta atawaongoza wenzake Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam

  Rais Malinzi amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Azam Complex, kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri.
  Taifa Stars itaingiaa kwenye mchezo huo ikitoka kwenye kambi ya wiki moja mjini Alexandria, Misri.
  Nahodha Mbwana Ally Samatta hakuwepo Misri na anatarajiwa kuungana na wenzake hapa Dar es Salaam akitokea Ubelgiji ambako anachezea klabu ya KRC Genk.
  Kiungo wa DC Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa AFC Eskilstuna ya Denmark, Thomas Ulimwengu wao walikuwepo Misri na wako tayari kwa mchezo wa keshokutwa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STARS NA MAMBA WA LESOTHO KUCHEZWA CHAMAZI USIKU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top