• HABARI MPYA

  Thursday, June 08, 2017

  SIMBA YAANZA KUFURU, YASAJILI WAWILI WA MWANZA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imeanza kuimarisha kikosi chake kelekea msimu ujao wa Kombe la Shirikisho la Afrika, baada ya leo kukamilisha usajili wa walinzi wawili kutoka Mwanza.
  Hao ni beki wa kushoto, Jamal Mwambeleko kutoka Mbao FC na beki wa kati Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans, zote za Mwanza.
  Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba, Mlipili amesaini miaka mitatu na Mwambeleko amesaini miaka miwili.
  Kifaa kipya; Makamu wa Rais, Geoffrey Nyange 'Kaburu' (kushoto) akisaini mkataba na beki Yussuf Mlipili (kulia) leo mjini Dar es Salaam 
  Anarudi nyumbani; Kaburu (kushoto) akisaini mikataba na beki Jamal Mwambeleko (kulia) ambaye amewahi kuchezea Simba B

  Amesema Mlipili anatua kwa mara ya kwanza kabisa Simba SC, wakati Mwambeleko amewahi kuchezea timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi.
  Na Kaburu ambaye anafahamika kwa jina la utani Perez, akifananishwa na Rais wa Real Madrid, Frorentino Perez amesema baada ya kukamilisha usajili wa wawili hao, wapenzi wa Simba wakae mkao wa kula kwa taarifa za kuvutia zaidi kuhusu usaili wa timu yao.
  “Kwa ujumla nina wachezaji sita ambao wamekwishakamilisha usajili wao hapa Simba, lakini nitakuwa nachomoa mmoja mmoja namtambukisha,”amesema.
  Mlipili na Mwambeleko wote waliichezea Simba SC kwa mara ya kwanza juzi ikitolewa kwa penalti 5-4 na Nakuru All Stars ya Kenya kwenye michuano ya SportPesa SuperCup baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAANZA KUFURU, YASAJILI WAWILI WA MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top