• HABARI MPYA

  Wednesday, June 07, 2017

  SHABIKI HUYU ALIANGUSHIWA 'JUMBA BOVU' DODOMA SIMBA NA MBAO

  Askari watatu wa Jeshi la Polisi wakiwa wamemtia nguvuni shabiki mtanashati Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakati fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Mei 27, mwaka huu, Simba ya Dar es Salaam ikishinda 2-1 dhidi ya Mbao ya Mwanza na kutwaa Kombe. Ilidaiwa shabiki huyo wa Simba alimtupia kitu kigumu shabiki wa Yanga aliyekuwa chini yake, lakini mbele ya askari alijitetea kwamba si yeye aliyefanya hivyo bali ni mtu mwingine aliyekuwa jirani yake
   Shabiki wa Simba akiwa amechonga msumeno kuwakejeli Mbao FC
  Huyu ni shabiki wa Yanga ambaye alikutana na adha ya kupigwa hadi kuchaniwa nguo kwa kukaa kwenye eneo walilokuwa wameketi mashabiki wengi wa Simba
  Askari Polisi akimkokota mbwa wake kufanya doria uwanjani
  Mashabiki wa Mbao FC pamoja na uchache wao, lakini walikuwa kivutio kwa staili yao ya kushangilia na vyungu vya moto huku wamejipaka chokaa 

  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHABIKI HUYU ALIANGUSHIWA 'JUMBA BOVU' DODOMA SIMBA NA MBAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top