• HABARI MPYA

    Wednesday, June 14, 2017

    RATIBA LIGI KUU ENGLAND IKO MTAANI, CHELSEA KUANZA NA BURNLEY

    Mabingwa watetezi, Chelsea wataanza msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa kumenyana na Burnley Agosti 12 GONGA HAPA KUTAZAMA RATIBA KAMILI 
       

    MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU YA ENGLAND AGOSTI 12, 2017

    Arsenal v Leicester City
    Brighton v Manchester City
    Chelsea v Burnley
    Crystal Palace v Huddersfield Town
    Everton v Stoke City
    Manchester United v West Ham United
    Newcastle United v Tottenham
    Southampton v Swansea City
    Watford v Liverpool
    West Bromwich Albion v Bournemouth
    MABINGWA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea wataanza kutetea taji lao kwa kumenyana na Burnley Uwanja wa Stamford Bridge, London Agosti 12.
    Kikosi cha Antonio Conte kitafuatiwa na mchezo dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Tottenham Uwanja wa Wembley katika marudio ya Nusu Fainali ya Kombe la FA msimu uliopita.
    Kikosi cha Jose Mourinho cha Manchester United kitawakaribisha West Ham Uwanja wa Old Trafford katika mechi ya ufunguzi, wakati jirani zao, City watasafiri hadi Uwanja wa Amex kjuwafuata wageni, Brighton.
    Arsene Wenger ataanza msimu mpya na Arsenal yake kwa kumenyana na Leicester City, wakati Liverpool itasafiri kuwafuata Watford katika mchezo wa kwanza wa Marco Silva kazini Vicarage Road.
    Spurs itakwenda Uwanja wa St James' Park kwa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Newcastle United, ambao mechi iliyopita ya Ligi Kuu walishinda 5-1 dhidi ya timu ya Mauriccio Pochettino. 
    Wageni wa Ligi Kuu, Huddersfield Town watawafuata Crystal Palace, na Newcastle watazuru Uwanja wa John Smith wiki moja baadaye kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu nyumbani ndani ya miaka 45.
    Southampton itamenyana na Swansea City Uwanja wa St Mary's wakati West Bromwich Albion wataikaribisha Bournemouth Uwanja wa The Hawthorns na Everton wataanzia nyumbani kwa Stoke City.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RATIBA LIGI KUU ENGLAND IKO MTAANI, CHELSEA KUANZA NA BURNLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top