• HABARI MPYA

    Tuesday, June 13, 2017

    NAHODHA SERENGETI BOYS, MAKAMBA AWASUTA ‘WASHAKUNAKU’ WANAOPAKAZA ETI TFF IMEMTELEKEZA NA MAGONGO YAKE

    Na Shekha Jamal, DARC ES SALAAM 
    NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys Issa Abdi Makamba ameshukuru kwa huduma anazoendelea kupatiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati huu akiwa majeruhi.
    Makamba aliumia kwenye kambi ya mazoezi ya Serengeti Boys nchini Morocco mwezi Aprili kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon Mei.
    Lakini alikwenda kwenye kambi ya Cameroon na baadaye kwenye fainali za AFCON U-17 nchini Gabon, ambako Serengeti Boys ilitolewa hatua ya makundi.
    Issa Makamba akiwa na wadogo zake nyumbani kwao Dodoma ambako anaishi 
    Issa Abdi Makamba akiwa mazoezini na Serengeti Boys kabla ya kuumia

    Kufuatia kurejea nyumbani, kukaibuka habari kwamba Nahodha huyo ametelekezwa na TFF, jambo ambalo leo amekana.
    “Ninapata simu nyingi sana juu yangu kuwa nimetelekezwa na TFF na kuna taarifa nying sana zinaenea kuhusu mimi. Ukweli ni kwamba, hapana mimi sijatelekezwa na TFF,” amesema Makamba. 
    “Na kuhusu suala la kwenda Dodoma ni kwetu na wazazi wangu ndiyo wanapoishi, hivyo kwenda kuwasalimia wazazi wangu imekuwa chanzo cha vitu vyote hivi. Mimi nipo sawa na ninaendelea vizuri sana tu,”amesema.
    Kwa ujumla wachezaji wote wa Serengeti Boys wapo chini ya uangalizi mzuri wa TFF baada ya fainali za Gabon kwa sababu wanaandaliwa kuwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAHODHA SERENGETI BOYS, MAKAMBA AWASUTA ‘WASHAKUNAKU’ WANAOPAKAZA ETI TFF IMEMTELEKEZA NA MAGONGO YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top