• HABARI MPYA

  Wednesday, June 14, 2017

  MTIBWA SUGAR KUINGIA KAMBINI JULAI, KUANZA NA MBEYA CITY

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro inatarajiwa kuingia kambini mapema Julai kuanza maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtibwa Sugar, Jamal Byser amesema kwamba baada ya mazoezi makali ya kukiamsha kikosi, timu itapata mchezo wa kwanza wa kujiandaa na msimu kwa kumenyana na Mbeya City Julai 29, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
  Bayser amesema kwamba mchezo dhidi ya Mbeya City umeandaliwa na kanisa la Faith Baptist na utafanyika kwa mara ya tatu mwaka huu, huku Mtibwa wakiwa wamewahi kushinda mara mbili ikiwemo mwaka jana baina ya timu hizo pia.
  Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Stahmili Mbonde (kushoto) akikimbilia mpira dhidi ya kiungo wa Simba, Jonas Mkude msimu uliopita 

  “Wachezaji kwa sasa wapo mapumzikoni baada ya ligi kuisha na Mtibwa tunatatarajia kuingia kambini mwezi wa saba mwanzoni, na katika kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao tayari tumepata mchezo mmoja dhidi ya Mbeya City wa maandalizi kwa ajili ya msimu ujao na tutawajuza michezo mingine ya kirafiki tutacheza na nani na wapi,” alisema Bayser.
  Pamoja na hayo, Bayser amesema kwamba uongozi upo katika mchakato wa usajili, ambao unafanywa kwa umakini mkubwa kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi.
  Amesema kwamba tayari wamepokea mapendekezo ya usajili kutoka kwenye taarifa ya benchi la ufundi iliyokabidhiwa na kocha Mkuu, Zubeiry Katwila mwezi uliopita mjini Dar es Salaam.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR KUINGIA KAMBINI JULAI, KUANZA NA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top