• HABARI MPYA

  Friday, June 09, 2017

  MESSI AFUATA NYAYO ZA RONALDO, ANUNUA HOTELI LA KIFAHARI BARCELONA

  NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi ameunua hoteli ya nyota nne katika eneo la ufukweni katikati ya Jiji la hilo la Katalunya.
  Muargentina huyo amenunua hoteli ya kifahari, yenye vyumba 77, kwa Euro Milioni 30, kwa mujibu wa gazeti la Expansion la Hispania.
  Hoteli hiyo yenye mwonekano mzuri, iliyo kwenye mandhari nzuri, ipo karibu na ufukwe na mbele ya bahari eneo la Sitges, umbali wa kilomita 40 kutoka Barcelona.

  Lionel Messi amenunua hoteli ya nyota nne, MiM iliyopo mjini tu eneo Sitges ufukweni mwa bahariPICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  Hivi karibuni ameibadilisha jina hoteli hiyo iliyojengwa mwaka 2013 na kuwa MiM, huku bei ya chumba ni kati ya Euro 250 hadi 300 kwa usiku mmoja.
  Mshambuliaji huyo wa Barcelona hivi karibuni ametambulisha kampuni yake mpya ya uwekezaji kwenye hoteli na apartments ikienda kwa jina la Rosotel, ambayo Messi ni Rais na kaka yake, Rodrigo ni kiongozi.
  Messi anafuata nyayo za Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo kwenye kununua hoteli - kwani nyota huyo wa Real Madrid kwa sasa anamiliki hoteli nne zenye thamani ya jumla ya Pauni Milioni 54.
  Hoteli hizo zipo katika majiji matatu: Funchal, Lisbon na Madrid – na nyingine New York.
  Mwezi Oktoba, mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ureno alizindua rasmi bendera ya hoteli zake zijulikanazo kama 'Pestana CR7 Lisboa' nyumbani kwao.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AFUATA NYAYO ZA RONALDO, ANUNUA HOTELI LA KIFAHARI BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top