• HABARI MPYA

  Thursday, June 08, 2017

  MASHEMEJI KATIKA FAINALI KALI YA SPORTPESA SUPER CUP 2017

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  FAINALI ya michuano ya SportPesa Super Cup itawakutanisha ‘Mashemeji wa Kenya’ Gor Mahia na AFC Leopards Jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Hiyo inafuatia Gor Mahia kuitoa Nakuru All Stars ya Kenya pia kwa mabao 2-0 katika Nusu Fainali ya pili jioni ya leo Uwanja wa Uhuru.
  Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Media Kagere dakika ya 45 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Timoth Otieno na George Odhiambo dakika ya 81 akimalizia kazi nzuri ya Haroun Shakava.
  Medie Kagere amefikisha mabao matatu kwenye SportPesa Super Cup
  Mapema katika Nusu Fainali ya kwanza, AFC Leopards iliitoa Yanga SC ya Tanzania kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  Bingwa wa michuano hii iliyoanza Juni 5 atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani, 30,000 zaidi ya Sh. Milioni 65 na nafasi ya kucheza na Everton ya England Julai 13, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kikosi cha Gor Mahia kilikuwa; Fredrick Othiambo, Haron Shakava, Innocent Wafula, Wellington Ochieng, Joach Onyango, Philemon Otieno, Francis Kahata, Kenneth Muguna, Timothy Otieno, Medie Kagere na Geogre Othiambo.
  Nakuru All Stars; Martin Lule, Antony Nganga, Njenga Wanaina/Baraka Nturukundo dk3, Omondi Siwa, Sadick Mukhwana, Ekuba Amakanji, Kamau Ng'ang'a, Sosi Nandwa, Amani Kyata, Godfrey Maina na Ndungu Kamau.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHEMEJI KATIKA FAINALI KALI YA SPORTPESA SUPER CUP 2017 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top