• HABARI MPYA

  Friday, June 09, 2017

  MAN UNITED YAHAMIA MORATA, IKO TAYARI KJTOA PAUNI MILIONI 60

  TIMU ya Manchester United ipo karibu kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata na inaweza kutoa hadi Pauni Milioni 60 kumpata mchezaji huyo.
  Nyota huyo wa Hispania atawaacha mabingwa hao wa Ulaya msimu unaofuata baada ya kufikia makubaliano ya vipengele vya maslahi yake binafasi.
  Jose Mourinho ameelekeza nguvu katika kumsajili namba 9 mpya huku United ikiwa haina mpango wa kumuongezea mkataba mkongwe majeruhi, Zlatan Ibrahimovic.
  Na huku mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku aliyekuwa anatakiwa pia na Mourinho kuwa mbioni kurejea Chelsea kwa dau la rekodi Uingereza, Morata anabaki kuwa mtu sahihi kwenda Old Trafford.

  Mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata anatakiwa na Manchester United PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Kwa muda mrefu United imeonyesha nia ya kumtaka Morata - ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni huko Ibiza na mpenzi wake, Alice Campello - na inaweza kutoa hadi Pauni Milioni 60 kumpata mchezaji huyo.
  Lukaku anaweza kuchagua kurejea Chelsea ambako klabu hiyo ya magharibi mwa London inajiandaa kuachana na mshambuliaji Diego Costa aliyetofautiana na kocha Antonio Conte.
  Morata alifanya kazi chini ya Jose Mourinho baada ya kuibuka kutoka timu ya vijana ya Real Madrid. Vigogo hao wa Hispania walimsajili tena mshambuliaji huyo baada ya kumuuza Juventus.
  Ibrahimovic, wakati huo huo, anaendelea na mazoezi katika viwanja vya mazoezi vya klabu, Carrington ingawa hajapata mkataba mpya.
  Gwiji huyo wa Sweden aliumia mguu Aprili mwaka huu katika mechi ya Europa League dhidi ya Ajax na anatarajiwa kuwa nje Januari mwakani.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAHAMIA MORATA, IKO TAYARI KJTOA PAUNI MILIONI 60 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top