• HABARI MPYA

  Wednesday, June 07, 2017

  LUKAKU AWAPITA WIMA MAN UNITED, ANATAKA KURUDI CHELSEA

  MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku amewaambia washauri wake kufuatilia uwezekano wa kurejea Chelsea msimu ujao.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anataka kuondoka Everton, huku Manchester United piaa nayo ikiwania saini yake.
  Lakini Lukaku amemuambia Mino Raiola nia yake ni kurejea Chelsea, klabu aliyoondoka kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 28 mwaka 2014.
  "Kubaki Everton si suluhisho tena kwa msimu ujao. Naendelea kutulia," amesema Lukaku mwenye umri wa miaka 24. "Hakuna kinachoendelea katika klabu (Everton) kwa sasa, wakala wangu ametingwa na mijadala,".

  Romelu Lukaku amewaambia washauri wake kushughulikia maongo wa kurejea Chelsea msimu ujao PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  "Siendi kufanya maamuzi makubwa kuhusu mustakabali wangu, lakini nafahamu wapi nataka kucheza: katika klabu ambayo inawania taji la Ligi ya Mabingwa na inaweza kushinda mataji England,"amesema.
  "Kwa sasa tupo kwenye mazungumzo na klabu na ninaangalia mbele. Wakala wangu anafahamu nini kitatokea na ninafahamu pia. Kazi bado inatakiwa kufanywa kabla ya Lukaku kutimiza matarajio yake,".
  Kikwazo kinatarajiwa kuw ada ambayo Everton itataka kumuuza Lukaku kurudi Chelsea, Pauni Milioni 100 ambayo itakuwa ni dau la rekodi ya dunia. Kukubaliana kwenye vipengele binafsi haitasumbua.
  "Naendelea kuwa mtulivu na tuna makubaliano na klabu pia,"alisema. "Ninakwenda kupumzika kwa siku chache na kisha kujiandaa kwa msimu ujao. Nataka kupata muda wa kupumzika, kubadilisha kila kitu katika kiwango kingine na kuwa bora zaidi ya nilivyokuwa mwaka jana. bado tumetulia na angalau tuna mwelekeo wapi tunataka kwenda,".
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AWAPITA WIMA MAN UNITED, ANATAKA KURUDI CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top