• HABARI MPYA

  Tuesday, June 13, 2017

  KOCHA MSUMBIJI ASEMA SASA MAMBAS TISHA MBAYA

  KOCHA wa Msumbiji, Abel 'Mamvi' Xavier amesema kwamba ushindi wa Mambas wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa Afrika mwaka 2012, Zambia katika mechi ya kwanza ya Kundi K kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 ni kielelezo cha ubora wa timu yao.
  Ushindi huo wa Mambas kuliotokana na bao pekee la Stanley Ratifo katika mchezo uliofanyika mjini Ndola Jumamosi, unakuwa wa kwanza kabisa dhidi ya Chipolopolo katika mechi 20 walizokutana.
  Xavier amesema kwamba baada ya kuwa kocha wa Msumbiji, ameonyesha kwamba kila kitu kinawezekana kwenye soka wakipigania kurudi kwenye Fainali za Mataifa baada ya kukosekana kwa miaka saba.
  Abel Xavier amesema ushindi wa Mambas wa 1-0 dhidi ya Zambiani kielelezo cha ubora wa timu yao

  "Ninajivunia wachezaji wangu baada ya kufanya kazi na timu kwa mwaka mmoja na nusu na kubadilisha mabo hadi yanakiuwa hivi,".
  Msumbiji itawania ushindi wa pili katika mechi za kili Machi mwakani, watakapomenyana na vinara wenzao wa Kundi K, Guinea Bissau ambao waliwafunga Namibia 1-0 nyumbani katika mchezo wa kwanza mjini Bissau.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MSUMBIJI ASEMA SASA MAMBAS TISHA MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top