• HABARI MPYA

    Tuesday, June 06, 2017

    KINDA WA YANGA NA SERENGETI BOYS ALIVYOMTESA MKONGWE WA TUSKER JANA

    Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Said Mussa akimtoka kwa chenga ya hatari beki wa Tusker ya Kenya, Collins Shivachi hadi kiatu kikamvuka katika mchezo wa SportPesa Super Cup jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Yanga ilishinda kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90
    Kiungo huyo aliyekuwamo kwenye kikosi cha timu ya vijana ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki michuano ya Afrika mwezi uliopita nchini Gabon alimtesa mno beki huyu wa Harambee Stars, timu ya taifa ya Kenya
    Ikafika wakati ikabidi Collins Shivachi ajaribu kumshika Said Mussa ili kumtuliza
    Lakini bado kijana alijinasua na kuendeleza safari yake
    Hapa kijana anajaribu kujinasua baada ya kushikwa jezi na Shivachi
    Mtu mzima wa Kenya ikabidi acheze hadi rafu kujaribu kumpokonya mpira kinda wa Jangwani
    Lakini dogo miguu yake kama ina sumaku inayonasa mpira 
     Aliinuka na akachukua mpira wake na kuanza kuondoka nao
    Jitihada za Mkenya kujaribu kumzuia kijana huyo hazikufanikiwa
    Alijaribu kumvuta tena jezi, lakini hakufanikiwa kijana akaambaa na mpira na kuacha mashabiki wakimpigia makofi mengi jukwaani
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KINDA WA YANGA NA SERENGETI BOYS ALIVYOMTESA MKONGWE WA TUSKER JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top