• HABARI MPYA

  Sunday, June 11, 2017

  KAPOMBE AWAKIMBIA VIONGOZI AZAM, AENDA KUSAINI SIMBA

  Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
  BEKI Shomari Salum Kapombe ni mchezaji wa tatu kutoka Azam FC kwenda Simba, baada ya kipa Aishi Salum Manula na mshambuliaji John Raphael Bocco.
  Kapombe amechukua maamuzi magumu leo, baada ya kuwakimbia viongozi wa Azam FC na kwenda kusaini Simba SC mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh. Milioni 50.
  Kapombe alitua Azam FC miaka miwili iliyopita kutoka AS Cannes ya Daraja la Nne Ufaransa, ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka Simba SC.
  Katika biashara hiyo, Simba ilipatiwa Sh. Milioni 60 na Azam FC mbali na Euro 43,000 ambazo ililipwa AS Cannes na wakala Dennis Kadito akapewa asilimia 20. 
  Rais wa Simba SC, Evans Aveva (kushoto) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, beki Shomary Kapombe baada ya kusaini mkataba wa kurejea nyumbani 

  Shomari Kapombe amekuwa mchezaji mwinginewa Azam kusaini Simba baada ya Aishi Manula na John Bocco  

  Kadito ndiye aliyempeleka Ufaransa Kapombe baada ya Simba SC kukubali kumtoa bure, kwa matarajio akiuzwa Ulaya itapata mgawo mzuri.
  Simba ipo katika harakati za kuimarisha kikosi chake baada ya kufanikiwa kurejea kwenye michuano ya Afrika msimu ujao.
  Na mbali ba Manula, Kapombe na Bocco Wekundu hao wa Msimbazi wana mpango wa kusajili nyota wengine kadhaa, akiwemo mshambuliaji wake wa zamani, Mganda Emmanuel Okwi.
  Na tayari Simba imewasili pia mabeki Jamal Mwambeleko kutoka Mbao FC na Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans, zote za Mwanza.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAPOMBE AWAKIMBIA VIONGOZI AZAM, AENDA KUSAINI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top