• HABARI MPYA

  Monday, June 12, 2017

  KAMUSOKO ANG'ARA, MUSONA APIGA TATU ZIMBABWE YAUA 3-0

  MSHAMBULIAJI Knowledge Musona jana ameiongoza Zimbabwe kwa mara ya kwanza kama Nahodha na kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Liberia mjini Harare.
  Katika mechi hiyo ya Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, kiungo wa Yanga ya Tanzania, Thabani Kamusoko alicheza vizuri na kutoa mchango kwenye ushindi huo.
  Ilikuwa ni siku ya furaha kwa Ghana pia baada ya kuichapa Ethiopia 5-0 katika mbio za Cameroon 2019.
  hat trick ya Musona inaipeleka Zimbabwe kileleni mwa Kundi G kwa tofauti ya wastani wa mabao na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo Jumamosi iliwafunga jirani zao, Kongo Brazzaville 3-1 mjini Kinshasa.
  Musona anayecheza Ubelgiji, anakuwa Nahodha wa kwanza wa Zimbabwe tangu Peter Ndlovu mwaka 2004 kufunga hat-trick timu ya taifa wakiichapa Liberia 3-0.
  Alifunga mabao hayo dakika za 24 baada ya kubaki na kipa Boison Wynney, dakika ya 50 akimalizia pasi ya Kudakwashe Mahachi na 63 baada ya kazi nzuri ya Kamusoko.
  Mabao ya Ghana yalifungwa na mkongwe Asamoah Gyan dakika ya 10, John Boye, Ebenezer Ofori na Raphael Dwamena mawili, huo ukiwa mwanzo mzuri kwa kocha Kwesi Appiah akipewa nafasi ya kufundisha Ghana kwa mara ya pili baada ya kutolewa Raundi ya kwanza kwenye Kombe la Dunia Brazil mwaka 2014.
  Ushindi huo unaipeleka Ghana kileleni mwa Kundi Kundi F kwa tofauti ya mabao na Sierra Leone, ambao waliifunga Kenya 2-1 jana.
  Knowledge Musona akiondoka na mpira baada ya kufunga mabao yote matatu Zimbabwe ikishinda 3-0 dhidi ya Liberia nyumbani

  MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA MWANZO KUFUZU AFCON 2019
  Juni 12, 2017  
  Tunisia 1 - 0 Misri
  Juni 11, 2017  
  Algeria 1 - 0 Togo
  Cape Verde 0 - 1 Uganda
  Cape Verde 0 - 1 Uganda
  Ghana 5 - 0 Ethiopia
  Benin 1 - 0 Gambia
  Jamhuri ya Afrika ya Kati  2 - 1 Rwanda
  Zimbabwe 3 - 0 Liberia
  Senegal 3 - 0 Equatorial Guinea
  Juni 10, 20117  
  Mali 2 - 1 Gabon
  Burkina Faso 3 - 1 Angola
  Ivory Coast 2 - 3 Guinea
  DRC 3 - 1 Kongo
  Tanzania 1 - 1 Lesotho
  Sierra Leone 2 - 1 Kenya
  Guinea-Bissau 1 - 0 Namibia
  Nigeria 0 - 2  Afrika Kusini
  Niger 0 - 0 Swaziland
  Cameroon 1 - 0 Morocco
  Botswana 0 - 1 Mauritania
  Zambia 0 - 1 Msumbiji
  Burundi 3 - 0 Sudan Kusini
  Malawi 1 - 0 Comoro
  Libya 5 - 1 Shelisheli
  Sudan 1 - 3 Madagascar
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMUSOKO ANG'ARA, MUSONA APIGA TATU ZIMBABWE YAUA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top