• HABARI MPYA

  Thursday, June 01, 2017

  JONAS MKUDE ALIVYOWAONGOZA WANAMICHEZO KUMUAGA MAREHEMU SHOSE LEO

  Nahodha wa Simba, Jonas Mkude akitoa heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Shose Fidelis, shabiki wa Simba aliyefariki baada ya ajali ya gari Jumapili Mei 28 eneo la Dumila, Morogoro akitokea Dodoma kuishangilia timu hiyo ikimenyana na Mbao FC katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC). Zoezi hilo lilifanyika katika Kanisa la Roman Catholic, Magomeni, Dar es Salaam na Mkude alikuwemo kwenye gari lililosababisha kifo cha Shose akitoka kuisaidia Simba kubeba Kombe la ASFC kwa ushindi wa 2-1, lakini yeye alinusurika 
  Mama mzazi wa marehemu Shose akilia mbele ya jeneza la binti yake
  Shabiki wa Yanga alishiriki msiba huo wa shabiki wa watani wao wa jadi
  Mdogo wa marehemu akilia kwenye jeneza la dada yake
  Rais wa Simba, Evans Aveva akipita mbele ya jeneza, akifuatiwa na makamu wake, Geoffrey Nyange 'Kaburu' 
  Kipa wa zamani wa Simba, Juma Kaseja (kushoto) ambaye kwa sasa anadakia Kagera Sugar alikuwepo pia. Mwili wa marehemu unasafirishwa leo kwenda Uru, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi kesho  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JONAS MKUDE ALIVYOWAONGOZA WANAMICHEZO KUMUAGA MAREHEMU SHOSE LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top