• HABARI MPYA

    Tuesday, June 13, 2017

    GRIEZMANN ASAINI MKATABA MPYA MNONO ATLETICO MADRID

    Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa, Antoine Griezmann amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu yake ya La Liga hadi mwaka 2022 PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    MKATABA MPYA WA GRIEZMANN KATIKA NAMBA 

    2022 - Mwaka ambao utamalizika 
    Pauni 88- Dau lake la kuuzwa
    Pauni 12.3 - Pato lake la msimu
    Pauni 235,000 - Malipo yake ya wiki
    1 - Atakuwa mchezaji namba moja kulipwa mshahara mkubwa na klabu hiyo
    3 - Idadi ya wachezaji wanaomzidi kupata mshahara mkubwa La Liga (Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar) 
    MSHAMBULIAJI Antoine Griezmann amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Atletico Madrid hadi mwaka 2022.
    Lakini Mfaransa huyo amepinga klabu hiyo kupandisha dau lake na sasa itaigharimu Manchester United Pauni Milioni 88 ile ile kama ada ya uhamisho iwapo itahitaji tena kumchukua mchezaji huyo mwaka ujao.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameingia pia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sasa akipoka Pauni 235,000 taslimu kwa wiki sawa na Pauni Milioni 12.3 kwa mwaka.
    Hiyo ni pungufu kidogo kutoka mshahara wa Pauni 300,000 ambao inafahamika Man United ilimuandalia. Lakini dili hilo linamfanya awe mchezaji anayelipwa zaisi Atletico Madrid na katika La Liga sasa anazidiwa na Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar kwa mshahara mkubwa.
    Atletico Madrid imelazimika kumpa ofa nzuri mchezaji huyo ili abaki baada ya kufungiwa kusajili na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hadi mwaka 2018.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GRIEZMANN ASAINI MKATABA MPYA MNONO ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top