• HABARI MPYA

  Saturday, June 10, 2017

  DIRISHA LA USAJILI BARA KUFUNGULIWA WIKI IJAYO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limekumbusha dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu ujao  wa mashindano wa 2017/2018 litafunguliwa Juni 15, mwaka huu.
  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, amesema kwamba baada ya kufunguliwa Juni 15, litafungwa Agosti 6, mwaka huu na ameitaka kila timu inayoshiriki michuano husika kufuata kalenda hiyo.
  “Tahadhali, hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu ambazo hazitakamilisha usajili kama ilivyotokea msimu uliopita kwa baadhi ya timu kushindwa kufanya kusajili kwa wakati na dirisha likafungwa,”amesema.
  Meneja wa Azam FC, Abdul Mohammed (kulia) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo Mbaraka Yussuf baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
  Wakati TFF inatangaza dirisha la usajili kufunguliwa wiki ijayo, tayari klabu mbalimbali zimekwishaanza kuingia mikataba na wachezaji.
  Simba SC imeingia mikataba na wachezaji wawili, wote mabeki Jamal Mwambeleko wa Mbao FC miaka miwili na Yussuf Mlipili wa Toto Africans, zote za Mwanza miaka mitatu.
  Azam FC imeingia mikataba na kiungo Salmin Hoza kutoka Mbao FC miaka miwili na washambuliaji, Waziri Junior kutoka Toto Africans na Mbaraka Yussuf kutoka Kagera Sugar wote miaka miwili.   
  Singida United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, nayo ni timu nyingine iliyoingia mikataba na wachezaji wengi.
  Timu nyingi zinatarajiwa kuingia rasmi sokoni kusaka wachezaji kuanzia wiki ijayo baada ya taarifa ya TFF kufungua dirisha la usajili.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIRISHA LA USAJILI BARA KUFUNGULIWA WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top