• HABARI MPYA

  Tuesday, June 13, 2017

  CISSE ALIVYOMWAGA MACHOZI AKiMUAGA TIOTE LEO BEIJING

  WACHEZAJI wenzake wa zamani na sasa wamejitokeza kuuga mwili mwa rafiki yao, Cheick Tiote, nyota wa zamani wa Newcastle United aliyefariki mapema mwezi huu.
  Tiote alifariki dunia akiwa mazoezini na klabu yake ya Beijing Enterprises ya China na leo kiungo huyo ameagwa.
  Mchezaji mwenzake wa zamani wa Newcastle, Muivory Coast mwenzake pia, Papiss Cisse alihudhuria zoezi hilo na akashindwa kujizuia kulia. "Nimeishi vizuri sana na huyu jamaa na leo ameondoka," alisema Cisse wakati wa kuaga huku akibubujikwa machozi. 
  Mwili wa mchezaji huyo aliyefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 30 utarejeshwa Ivory Coast kesho kwa mazishi.
  Papiss Cisse akibubujikwa machozi wakati wa kuaga mwili wa mchezaji mwenzake wa zamani, Cheick Tiote leo mjini Beijing, China  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CISSE ALIVYOMWAGA MACHOZI AKiMUAGA TIOTE LEO BEIJING Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top