• HABARI MPYA

  Monday, June 05, 2017

  TIOTE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZIMIA MAZOEZINI CHINA

  KIUNGO wa zamani wa Newcastle United, Cheick Tiote amefariki dunia akiwa ana umri miaka 30 baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China.
  Katika miaka yake saba ya kuwa Newcastle United, mchezaji huyo wa Ivory Coast amecheza mechi zaidi ya 150, zikiwemo tatu za msimu uliopita.
  Alijiunga na timu ya Daraja la Pili China, Beijing Enterprises kutoka Newcastle mwezi Februari.
  "Kwa masikitiko makubwa, nathibitisha kwamba Cheick Tiote kwa machungu amefariki dunia mapema leo baada ya kuzimia mazoezini,"amesema Msemaji, Emanuele Palladino.
  Cheick Tiote amefariki dunia leo akiwa ana umri miaka 30 baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China  

  "Hatuwezi kusema tena kwa sasa na tunaomba kwamba mambo ya faragha ya familia yake yaheshimiwe katika wakati huu mgumu. Tunaombeni dua zenu wote,".
  Mzaliwa huyo wa Ivory Coast, Tiote alikuwemo kwenye kikosi cha Ivory Cioast kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
  Kisoka aliibukia katika timu ya Anderlecht ya Ubelgiji mwaka 2005 kabla ya kuhamia FC Twente ya Uholanzi, ambako alicheza mechi 86 na kutwaa taji la Eredivisie msimu wa 2009- 2010 chini ya kocha Steve McClaren.
  Tiote, kiungo wa ulinzi hodari, alisaini Newcastle mwaka 2010 kwa dau la Pauni Milioni 3.5 na Februari mwaka 2011, alifunga bao la kukumbukwa Newcastle United ikitoka nyuma kwa mabao 4-0 na kutoa sare na Arsenal katika Ligi Kuu ya England.
  Hata hivyo, Februair mwaka huu alijiunga na Beijing Enterprises Group FC ambako ndiko umauti umemkuta. Mungu ampumzishe kwa amani Cheick Tiote.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIOTE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZIMIA MAZOEZINI CHINA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top