• HABARI MPYA

    Monday, June 05, 2017

    AZAM FC YAIPIGA BAO YANGA, YAMSAINI STRAIKA HATARI WA TOTO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Azam FC leo imemsaini kwa mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji hatari wa Toto Africans ya Mwanza, Wazir Junior aliyekuwa anawaniwa pia na Yanga SC.
    Mchezaji huyo ni pendekezo la Kocha Mkuu, Mromania Aristica Cioaba ambaye alivutiwa naye baada ya kumuona akiichezea Toto iliyoshuka Daraja dhidi ya Azam.
    Waziri aliyefunga mabao sita msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Azam kwa ajili ya msimu ujao 2017-18.
    Zoezi la kuingia mkataba kwa pande hizo mbili limefanyika leo mchana kwenye Ofisi za Mzizima, zilizopo barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, na kusimamiwa na Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, aliyekuwa sambamba na viongozi wengine Meneja wa timu, Phillip Alando na Ofisa Habari, Jaffar Idd.
    Waziri Junior (kushoto) akisaini mkataba wa kujiunga na Azam FC. Kulia ni Meneja wa Azam FC, Abdul Mohammed

    Azam FC ambayo imeanzisha falsafa ya kutengeneza timu ya muda mrefu yenye wachezaji vijana wenye vipaji pamoja na kuwekeza ipasavyo kwenye kituo chake cha kukuza vipaji ‘Azam Academy’ kwa kupandisha wachezaji bora, inaamini ya kuwa ujio wa mshambuliaji huyo utaongeza zaidi makali kwenye eneo la ushambuliaji.
    Mshambuliaji huyo anaungana na washambuliaji wengine kikosini, Yahaya Mohammed, Shaaban Idd, Samuel Afful na Yahaya Zaidi, aliyepandishwa kwenye timu kubwa kwa ajili ya msimu ujao akitokea katika kituo cha kukuza vipaji vya ‘Azam Academy’.
    Waziri Junior alifika hadi makao makuu ya Yanga katika mipango ya kujiunga na klabu hiyo, lakini baadaye akaenda kusaini Azam
    Wachezaji wengine ambao tayari wameongezwa kwenye timu kubwa kuelekea msimu ujao wakitokea kituo hicho, ni mabeki Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey Elias, kiraka Ramadhan Mohamed na kiungo Stanslaus Ladislaus.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA BAO YANGA, YAMSAINI STRAIKA HATARI WA TOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top