• HABARI MPYA

    Monday, June 05, 2017

    AL AHLY YAIPIGA WYDAD 2-0 NA KUONGOZA KUNDI D

    TIMU ya Al Ahly SC ya Misri jana imeichapa mabao 2-0 Wydad Athletic Club ya Morocco katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri.
    Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Moamen Zakaria dakika ya 24 na Junior Ajayi dakika ya 79 na sasa Ahly inapanda kileleni mwa kundi hilo, ikifikisha pointi saba sawa na Zanaco ya Zambia, inayozidiwa wastani wa mabao na Wamisri hao. 
    Uwanja wa Addis Ababa, Ethiopia bao pekee la Saladin Said dakika ya 60 lilitosha kuwapa wenyeji, Saint George ushindi wa 1-0 dhidi ya AS Vita.
    Etoile du Sahel juzi ilipunguzwa kasi katika Ligi ya Mabingwa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Al Hilal Omdurman Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse.
    Pamoja na matokeo hayo, vigogo hao wa Tunisia wanabaki kileleni mwa Kundi A wakiongoza kwa pointi tatu zaidi kufuatia ushindi wa Ferroviario Beira nyumbani mjini Maputo.
    Baada ya kipindi cha kwanza kigumu, Zied Boughattas akawafungia bao la kwanza washindi hao wa mwaka 2007 wa Ligi ya Mabingwa bao la kuongoza dakika ya 57.
    Timu ya Sudan ikafanikiwa kucheza mechi ya 24 bila kupoteza kwenye mashindano yote, baada ya kusawazisha bao hilo dakika ya 80 kupitia kwa Mohamed Musa mjinii Sousse.

    MATOKOE YOTE LIGI YA MABINGWA AFRIKA
    Juni 4, 2017  
    Al Ahly SC 2 - 0 Wydad Athletic Club
    Saint George 1 - 0 AS Vita Club
    Juni 3, 2017
    Etoile du Sahel 1 - 1 Al-Hilal
    Zanaco FC 2 - 1 Coton Sport
    Ferroviario Beira 1 - 0 Al Merrikh
    Juni 2, 2017
    Zamalek SC 1 - 1 USM Alger
    Mamelodi Sundowns 1 - 2 Esperance
    CAPS United 2 - 4 Al Ahli Tripoli
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AL AHLY YAIPIGA WYDAD 2-0 NA KUONGOZA KUNDI D Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top