• HABARI MPYA

  Tuesday, May 16, 2017

  YANGA CHEREKO CHEREKO…TAMBWE AWAUA TOTO TAIFA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  SHAMRASHAMRA za ubingwa zimeanza kurindima mitaa ya Jangwani, baada ya Yanga SC kuwachapa ‘watoto wao’, Toto Africans 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
  Ushindi huo uliotokana na bao pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Joselyn Tambwe unaifanya Yanga ifikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 29 na itahitaji sare tu kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mbao FC kujihakikishia taji la ubingwa.
  Lakini hata sasa, Yanga wanaweza kuanza kushangilia ubingwa kutokana na hazina kubwa ya mabao waliyonao, kwani sasa Simba watatakiwa kuifunga Mwadui FC mabao 13-0 ili kuizuia timu ya Jangwani kutwaa taji kla tatu la mfululizo.
  Amissi Tambwe ameendelea kuwa mchezaji muhimu Yanga SC 

  Katika mchezo wa leo, dakika 45 za kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu na Yanga walitangulia kupata nafasi ya wazi dakika ya tatu kupitia kwa mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliyepiga kichwa na beki ya Toto, Yussuf Mpili akaokoa mpira kaika eneo la hatari wakati tayaei kipa wao David Kissu amekwishondoka katika eneo lake.
  Dakika ya 38 Obrey Chirwa alitengeneza nafasi nzuri ya wazi, lakini shuti la kiungo Mzimbabwe Thaban Kamusoko likaokolewa na kipa wa Toto, Daviod Kisu na kuwa kona ambayo haikuwa na madhara.
  Dakika ya 44 mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe akaikosesha Yanga bao baada ya kupiga shuti hafifu akiwa kwenye nafasi nzuri.
  Lusajo Lerient naye aliipotezea nafasi Toto Africans dakika ya 22 baada ya kupiga nje akiwa kwenye nafasi nzuri. 
  Hussein Kasanga naye aakapoga vizuri shuti la mpira wa adhabu, lakini kipa wa Yanga, Benno Kaakolanya akaokoa na kuwa kona ambayo haikuwa na madhara.
  Mrundi Amissi Joselyn Tambwe akawainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 81 kwa kufunga bao kwa kichwa akimalizia krosi safi iliyopigwa na beki wa kulia, Juma Abdul Jaffar Mnyamani.   
  Dakika 79 Mwinyi Hajji Mngwali alitengeneza nafasi nzuri ya bao, lakini winga Emmanuel Martin aliyeingia kuchukua nafasi ya Geoffrey Mwashiuya alipiga shuti dhaifu na kipa wa Toto, Kisu akadaka.                             
  Kikosi cha Yanga kilikuwa; Beno Kakolanya, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondani, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi/Deus Kaseke dk46, Haruna Niyonzima/Justine Zulu dk89, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Geofrey Mwashiuya/Emmanuel Martin dk71.
  Toto Africans: David Kisu, Mohammed Soud/Wazir Ramadhani dk5, Reliant Lusajo, Hamim Abdul, Ramadhani Malima, Yusuf Mpili, Carlos Protas, Hussein Kasanga, Waziri Junior, Juvenary Pastory na Jaffar Mohamed.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA CHEREKO CHEREKO…TAMBWE AWAUA TOTO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top