• HABARI MPYA

  Tuesday, May 16, 2017

  WATANZANIA KAZINI KESHO AFCON U-17 GABON

  Na Mwandishi Wetu, LIBREVILLE
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limewateua Watanzania watatu kuwa maofisa waandamizi wa kusimamia mchezo wa kundi A kati ya  Ghana na Gabon wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 utakaofanyika Uwanja wa Port Gentil utakaofanyika kesho Mei 17, 2017.
  Watanzania hao ni Mwesigwa Joas Selestine atakayekuwa Kamisha wa mchezo huo wakati Frank John Komba atakuwa mwamuzi msaidizi na katika kitengo cha kitaalamu cha uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia dawa za kusisimua misuli atakuwa Dk. Paul Gasper Marealle.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na refa Frank Komba jana mjini Libreville

  Hii ni fahari kwa nchi yetu Tanzania kwa viongozi wake kuthaminiwa na kuaminika katika nyanja za kimataifa.
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawapongeza viongozi hao na inawatakia kila la kheri katika kutimiza majukumu waliyopangiwa kesho na baadaye hasa ikizingatiwa kuwa fainali zijazo za vijana kama hizi, zitafanyika Tanzania mwaka 2019.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WATANZANIA KAZINI KESHO AFCON U-17 GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top