• HABARI MPYA

    Thursday, May 11, 2017

    TAMBWE NA MAVUGO WOTE WAITWA INT’HAMBA MURUGAMBA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WASHAMBULIAJI Amissi Tambwe wa Yanga na Laudit Mavugo wa Simba za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wote wameitwa kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 35 wa timu yao ya taifa, Burundi kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon dhidi ya Sudan Kusini.
    Int’hamba Murugamba wamepangwa Kundi C kuwania tiketi ya AFCON 2019 na wataanzia nyumbani dhidi ya Bright Stars Juni 9, mwaka huu.
    Kocha wa Burundi, Olivier Niyungeko pia amemuita kikosini mshambuliaji wa Bloemfontein Celtic ya Afrika Kusini, Fiston Razak Abdul.
    Laudit Mavugo wa Simba ameitwa kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 35 wa Burundi kwa ajili ya mchezo na Sudan Kusini

    Mchezaji huyo wa zamani wa Sofapaka ya Kenya, alicheza vizuri Celtic ikitoa sare na Orlando Pirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini Jumatano usiku. Aidha, kiungo wa zamani wa Simba, Pierrot Kwizera anayechezea Rayon Sports ya Rwanda, naye pia amejumuishwa kikosini.
    Kikosi kamili cha Burundi ni; Nahimana Jonathan (Vital’o FC), Mutombora Fabien (LLB), Harerimana Rachid Léon (LLB), Ndaye Chancel (LLB), Barisize Nassor (Olympic Star), Habonimana Celestin Manyoka (LLB), Moussa Omar (Athletico Olympic), Ndoriyobija Eric (LLB), Nshimirimana David (Vital’o FC).
    Wengine ni Ndayisenga Franck Dunia (Musongati FC), Duhayindavyi Gael (Vital’o FC), 
    Urasenga Cedric Danny Kagabo (Messager Ngozi), Ntirwaza Sudi (Musongati FC), Barirengako Franck (Musongati FC), Sabumukama Enock (Messager Ngozi), Ndayishimiye Youssouf Nyange (Aigle Noir) na Ndikumana Tresor (LLB).
    Wamo poa Ndarusanze Jean-Claude Lambalamba/ (LLB), Mustapha Souleiman (Aigle Noir), Ndizeye Seif Thomson (LLB), Bimenyimana Bonfils Caleb (Vital’o FC), Hakizimana Alexis Kitenge (Athletico Olympic), Niyonkuru Pascal (LLB), Ulimwengu Jules (Vital’o FC), Wilondja Ismaïl Semele (Messager Ngozi), Abakinyi Bazoza Bavuye (Hanze y’igihugu), Amissi Cedric (Clube Madeira, Ureno), Bigirimana Gael (Coventry/Grande Bretagne), Ndikumana Selemani (Qatar), Abdoul Razzak Fiston (Celtic Bloemfontein, Afrika Kusini), Nsabimana Frederic (Jomo Cosmos, Afrika Kusini), Nizigiyimana Abdoul Karim (Gor Mahia, Kenya), Mavugo Laudit (Simba SC), Amissi Tambwe (Yanga), Nahimana Shassir (Rayon Sport na Kwizera Pierre (Rayon Sport).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAMBWE NA MAVUGO WOTE WAITWA INT’HAMBA MURUGAMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top