• HABARI MPYA

    Sunday, May 14, 2017

    SINGIDA UNITED YAMSAINI MSHAMBULIAJI WA MAMELODI ALIYEWAFUNGA MAZEMBE

    Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
    SINGIDA United imeendelea kujiimarisha kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa zamani wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Nhivi Simbarashe, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Caps United ya nchini Zimbabwe.
    Mchezaji huyo wa zamano SuperSport United ya Afrika Kusini pia, anakuja Singida United iliyopanda Ligi Kuu msimu baada ya kumaliza mkataba wake Caps United.
    Simbarashe anakumbukwa zaidi kutokana na kuifungia bao pekee Mamelodi ikiifunga TP Mazembe 1-0 na kuitipa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
    Sanga Festo (kushoto) akimkabidhi jezi Nhivi Simbarashe baada ya kusaini mkataba leo. Na Picha ya chini ni wakati anasaini
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Singida, Festo Sanga, alisema wameamua kumsajili mchezaji huyo baada ya kuvutiwa na kiwango chake kizuri hivyo wanaamini ataisaidia timu yao kupata matokeo mazuri katika Ligi msimu ujao.
    “Leo (jana), tuliingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo kutoka klabu ya Cups United, ambaye aliwahi kuzichezea timu za Super Sport na Mamelodi Sundowins zote zikiwa za Afrika Kusini,” alisema.
    Alisema usajili huo unaonyesha wazi kuwa hawakuja ligi kuu kushiriki bali kutafuta ubingwa na baadaye kwenda kwenye ligi ya mabingwa Afrika.
    Usajili wa mchezani huyo ufanya idadi ya wachezaji watano wa kimataifa ambapo tayari wameshamsajili wazimbabwe, Twafaza Kutinyu, Elisha Muroiwa,Wisdom Mtasa na Mganda Shafik Batambuze.     
    Singida ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja msimu huu kwa ajili ya kushiriki Ligi Kuu msimu ujao pamoja na timu za Njombe Mji na Lipuli FC za Iringa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAMSAINI MSHAMBULIAJI WA MAMELODI ALIYEWAFUNGA MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top