• HABARI MPYA

  Saturday, May 20, 2017

  SIMBA ‘WAZUIA’ SHEREHE ZA UBINGWA YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inasambaza vilelezo kwamba imepeleka malalamiko Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudai wapewe pointi tatu walizopokonywa, ambazo wakifanikiwa kurejeshewa watakuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Ligi Kuu imefikia tamati leo na Yanga SC wametawazwa tena kuwa mabingwa kwa wastani wao mzuri wa mabao licha ya kufungana kwa pointi na Simba SC, 68 kila moja baada ya mechi 30 za msimu.
  Lakini Simba wanataka waikumbushie Yanga machungu ya mwaka 2000 walipofanikiwa kutwaa ubingwa kwa matokeo ya uwanjani, kabla ya baadaye aliyekuwa Waziri wa Michezo, Profesa Juma Kapuya kuwapa pointi za mezani Mtibwa Sugar wakawa mabingwa.
  Nakala iliyosainiwa na Katibu wa Simba, Hamisi Kisiwa inaonyesha barua hiyo ilitumwa Mei 17 kwa njia ya Fax na nakala yake wakapewa TFF.
  Ikumbukwe madai ya msingi ya Simba ni kurejeshewa pointi tatu walizopewa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 baada ya kuikatia rufaa Kagera Sugar kwa madai ya kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa anatumia adhabu ya kadi za tatu njano.
  Simba SC ilifungwa 2-1 katika mchezo huo uliofanyika Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, lakini Kamati ya Saa 72 ikawpa pointi tatu za mezani. Hata hivyo, Kagera Sugar wakakata rufaa TFF wakisema mchezaji wao hakuwa ana kadi tatu, bali mbili na wakarejeshewa pointi zao.
  Simba nao sasa wameamua kusonga mbele hadi FIFA ili warejeshewe pointi zao na hatimaye kutimiza ndoto zao za kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.      
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA ‘WAZUIA’ SHEREHE ZA UBINGWA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top