• HABARI MPYA

    Friday, May 12, 2017

    SIMBA KUREJEA KILELENI LEO?

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    USUKANI wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaweza kurejea mikononi mwa Simba SC iwapo wataifunga Stand United jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Wekundu hao wa Msimbazi watacheza mechi yao ya 29 leo watakapowakaribisha Stand United, huku wakihitaji lazima kushinda ili kuweka hai matumaini ya ubingwa.
    Kwa sasa, Simba ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog ina pointi 62, sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao wapo kileleni kwa wastani wao mzuri wa mabao na pia wana mechi moja mkononi.
    Matokeo yoyote tofauti na ushindi, wazi yatawatoa Simba kwenye mbio za ubingwa na haswa kama Yanga nao watashinda kesho dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa.
    Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo ni kati ya wenyeji, Azam FC na Toto Africans Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wakati kesho mbali na Yanga kumenyana na Mbeya City, Mtibwa Sugar wataakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Mechi nyingine za kesho ni kati ya JKT Ruvu na Maji Maji ya Songea Uwanja wa Maji Maji, 
    Tanzania Prisons na Ndanda Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Jumapili African Lyon itamenyana na Ruvu Shooting.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA KUREJEA KILELENI LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top