• HABARI MPYA

  Friday, May 12, 2017

  SERENGETI YAREJESHA UDHAMINI TAIFA STARS, YAMWAGA BILIONI 2.1

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) leo imetangaza udhamini wa Sh. Bilioni 2.1 kwa miaka mitatu kwa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
  Hilo limefanyika jioni ya leo katika ukumbi wa Kivukoni 4, hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie amesema kwamba wanayo furaha kurejesha udhamini wao Taifa Stars.
  Mama huyo raia wa Uholanzi amesema kwamba ni matumaini yao sasa soka ya Tanzania itarudi juu tena kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baasa ya SBL kurejea.
  Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (katikati) wakiwa wameshika mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 2.1 kwa pamoja na Waziri wa Michezo, Dk Mwakyembe (kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) 


  Hii ni mara ya pili kwa SBL kuidhamini timu ya taifa baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2008 hadi 2011.
  Katika makubaliano hayo ambayo yalisainiwa leo na pande hizo mbili na Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie na Rais wa TFF Jamal Malinzi, kampuni ya SBL itapata fursa ya kutanga biashara yake wakati wa mechi zote za Taifa Stars za nyumbani na ugenini.
  Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo Bi Weesie alisema uamuzi wa kampuni hiyo wa kuidhamini timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya kusaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo. 
  ga mkono sekta ya michezo nchini na kubainisha kwamba  michezo sio tu inaburudisha bali pia inaunganisha mashabiki na pia ni chanzo cha kipato kwa vijana.
  “SBL inaona fahari kuidhamini timu yetu ya taifa kwa mara nyingine. Tumechukua hatua hiii kwa kuwa tunaelewa mchango wa sekta michezo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kukuza vipaji vya vijana wetu pamoja na kuleta hamasa kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya taifa,” alisema Weesie.
  Kwa upande wake, Rais wa TFF aliishukuru SBL kwa kukubali kuidhamini Taifa Stars jambo ambalo alisema litasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani nan je ya nchi.
   “Udhamini wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo katika hatua za  maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.
  Hafla ya kusainiwa kwa udhamini huo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe ambaye  alitoa wito kwa  kampuni zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI YAREJESHA UDHAMINI TAIFA STARS, YAMWAGA BILIONI 2.1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top