• HABARI MPYA

  Thursday, May 18, 2017

  SERENGETI BOYS YAPIGA HONI KOMBE LA DUNIA, YAILAZA 2-1 ANGOLA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  TANZANIA imepiga honi Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 17 Oktoba mwaka India, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angola jioni ya leo katika mchezo wa Kundi B Fainali za U-17 Afrika Uwanja wa L’Amittee mjini Libreville, Gabon.
  Ushindi huo unaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi nne na kukaa juu ya Kundi B, baada ya kucheza mechi mbili, ya kwanza ikitoa sare ya 0-0 na Angola Jumatatu wiki hii.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na Abou Coulibaly kutoka Ivory Coast aliytesaidiwa na 
  Mamady Tere wa Guinea na Attia Amsaad wa Libya, hadi mapumziko kila timu ilikuwa ina bao moja.
  Kevin Nashon Naftali akiwa juu kupiga kichwa kuifungia Serengeti Boys bao la kwanza
  Enrick Vitalis Nkosi wa Serengeti Boys (kulia) akiwania mpira dhidi ya Miguel Anselmo Basilio Daniel wa Angola
  Nickson Kibabage wa Serengeti Boys akipiga krosi pembeni ya Jelson Joao Mivo wa Angola

  Wachezaji wa Tanzania wakishangilia bao la kwanza leo Uwanja wa L'Amittee mjini Libreville

  Tanzania walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake tegemeo Yohana Oscar Mkomola dakika ya tano kwa kichwa baada ya krosi ya Enrick Vitalis Nkosi kabla ya Francisco Chilumbo kuisawazishia Angola dakika ya 19.
  Serengeti Boys ingeweza kumaliza kipindi cha kwanza inaongoza kwa mabao zaidi, kama wachezaji wake wangekuwa makini katika kutumia nafasi walizotengeneza.
  Kipindi cha pili, nyota ya Serengeti Boys iliendelea kung’ara, lakini tatizo likabaki kuwa umalizijia wa nafasi walizokuwa wakitengeneza.
  Hata hivyo, Abdul Suleiman awapa raha Watanzania kwa kufunga bao zuri la ushindi dakika ya 69 akimalizia pasi ya Yohanna Oscar Nkomola.
  Angalau pasi ya bao aliyotoa mwa Abdul itamfariji Nkomola, kwani ndiye mchezaji aliyepoteza nafasi nyingi za mabao leo. 
  Serengeti Boys itashuka tena dimbani Mei 21 kucheza mechi yake ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Niger, ambayo leo inamenyana na mabingwa watetezi, Mali. Timu zitakazoingia Nusu Fainali zitafuzu moja kwa moja fainali za Kombe la Dunia.
  Kikosi cha Tanzania leo kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Ally Ng'anzi, Nickson Kibabage, Enrick Nkosi/Said Bakari dk45/Shaaban Ada dk52, Dickson Job, Abdul Suleiman, Asad Ali/Muhsin Makame dk78, Kibwana Ally, Ally Msengi, Yohana Mkomola na Kelvin Naftal.
  Angola; Nsesani Emanuel Simao, Miguel Anselmo Basílio Daniel, Euclides Moisés Fernando Dos Santos, Fiete Quintas Agostinho Dos Santos, Orlando Luís Secali, Jelson João Mivo, Pedro Agostinho, Melono Muondo Dala, Adalmiro Patrício Pacheco Da Silva, Francisco Chilumbo na Moises Amor.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAPIGA HONI KOMBE LA DUNIA, YAILAZA 2-1 ANGOLA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top