• HABARI MPYA

    Monday, May 15, 2017

    SERENGETI BOYS YAANZA KWA SARE NA MABINGWA WATETEZI

    Na Mahmoud Zubeiry, LIBREVILLE
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imegawana pointi na mabingwa watetezi, Mali katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Fainali za Mataifa ya Afrika jioni ya leo Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville, Gabon.
    Ulikuwa mchezo kama mkali kama ilivyotarajiwa na Mali ndiyo walioutawala zaidi nap engine kutokana na wapinzani wao kucheza kwa tahadhari ya kujihami zaidi.
    Mali walimiliki mpira kwa muda mrefu na kupanga vyema mashambulizi yao, lakini safu ya ulinzi ya Tanzania ilicheza vizuri na kuokoa hatari nyingi ukiacha chache ambazo mabingwa hao watetezi walipoteza wenyewe.
    Abdul Suleiman akiwa amebaki na kipa wa Mali, Alkalifa Koulibaly lakini akashindwa kufunga
    Wachezaji wa Mali na Tanzania wakiwania mpira wa juu
    Yohana Oscar Nkomola wa Serengeti Boys akimiliki mpira mbele ya beki wa Mali

     Sifa zaidi zimuendee kipa wa Tanzania, Ramadhani Kabwili aliyeokoa michomo mingi ya hatari ya washambuliaji mafundi wa Gabon. 
    Kwa kutumia mfumo wa kushambulia kwa kushitukiza, Serengeti Boys nayo ililikaribia mara kadhaa lango la Mali, lakini wakashindwa kutumia nafasi.
    Na zaidi Serengeti Boys ilipata nafasi za kufunga kipindi cha pili, huku nafasi nzuri zaidi akiipoteza Abdul Suleiman ambaye akiwa amebaki na kipa wa Mali, Alkalifa Koulibaly kwenye akapiga ovyo mpira ukapotea.   
    Mchezo wa pili wa Kundi B unafuatia jioni hii kati ya Niger na Angola baada ya mechi za Kundi A kuchezwa jana Uwanja wa Port Gentil jana wenyeji Gabon wakifungwa mabao 5-1 na Guinea  huku Ghana wakianza vizuri kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Cameroon.
    Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Ally Ng'anzi, Nickson Kibabage, Dickson Nickson, Asad Ali, Mohamed Abdallah, Kibwana Ally, Shaban Zubeiry, Ally Msengi, Yohana Mkomola na Kelvin Nashon Naftal. 
    Mali; Youssouf Koita, Felix Kamate, Mamadi Fofana, Mohamed Camara, Seme Camara, Sibiry Keita, Abdoulaye Diaby, Mamadou Samake, Ibrahim Kane, Lassana N'diaye na Cheick Doucoure.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAANZA KWA SARE NA MABINGWA WATETEZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top