• HABARI MPYA

    Saturday, May 13, 2017

    MSUVA NA BAO LA KISHUJAA LILILOMTOA DAMU HADI KUSHONWA NYUZI NNE LEO

    Winga wa Yanga, Simon Msuva akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuchanika juu ya jicho la kushoto wakati akiifungia timu yake bao la kwanza dakika ya saba katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
    Hapa ndipo Msuva alipoumia wakati anapiga kichwa kufunga aligongana na beki wa Mbeya City, Tumba Lui Swedi
    Wachezaji wa Yanga wakiwaita watu wa huduma ya kwanza kuja kumsaidia Simon Msuva baada ya kuanguka chini
    Wachezaji wengine wa Yanga wakimsaidia Msuva, huku wengine wakiwaita watu wa huduma ya kwanza
    Hapa Msuva anatolewa nje ya Uwanja, kabla ya kupelekwa kwenye zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa kwa matibabu zaidi
    Alikuwa akipelekwa huku akifutwa damu kwenye jeraha lake
    Hapa Msuva akiwa kwenye Zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa baada ya matibabu na kushonwa nyuzi nne kwenye jeraha lake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA NA BAO LA KISHUJAA LILILOMTOA DAMU HADI KUSHONWA NYUZI NNE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top