• HABARI MPYA

  Tuesday, May 16, 2017

  'MSHKAJI' WAKE SAMATTA AWA MCHEZAJI BORA WA MSIMU LEICESTER CITY

  Kiungo Mnigeria, Wilfred Ndidi akiwa ameshika tuzo yake ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Msimu wa Leicester City baada ya kukabidhiwa jana Uwanja wa King Power. Ni mafanikio makubwa mchezaji huyo aliyejiunga na Leicester City Januari tu mwaka huu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji alipokuwa anacheza na Mtanzania, Mbwana Samatta. Kipa Kasper Schmeichel ameshinda tuzo mbili Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Msimu na Mchezaji Bora wa Mwaka kuonyesha umuhimu wake katika klabu hiyo. Nahodha Wes Morgan ameshinda tuzo ya Kiwango Bora cha Msimu alichoonyesha katika mechi dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa, Danny Drinkwater ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu alilofunga dhidi ya Liverpool kwenye ushindi wa 3-1 mwezi Machi wakati Harvey Barnes ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa kikosi cha pili na Alex Pascanu ni Mchezaji Bora wa Akademi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'MSHKAJI' WAKE SAMATTA AWA MCHEZAJI BORA WA MSIMU LEICESTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top