• HABARI MPYA

  Thursday, May 18, 2017

  GHANA YATINGA NUSU FAINALI, CAMEROON MGUU NJE

  Na Mwandishi Wetu, PORT GENTIL
  TIMU ya Ghana imekuwa ya kwanza kutinga Nusu fainali ya michuano ya vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17, baada ya kuwafunga wenyeji, Gabon mabao 5- 0 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Port Gentil leo. 
  Mshambuliaji na Nahodha, Eric Ayiah aliye katika kiwango kizuri na kiungo, Emmanuel Toku kila mmoja amefunga mabao mawili leo, wakati Patmos Arhin aliyetokea benchi kipindi cha pili akafunga linguine.
  Matokeo hayo yanamaanisha Ghana inafikisha pointi sita na mabao tisa baada ya Jumapili kushinda 4-0 dhidi ya Cameroon katika mchezo wake wa kwanza.
  Maana yake pia Ghana wamejikatia tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia za U-17 baadaye mwaka huu, wakati wenyeji wanapoteza nafasi ya kusonga mbele baada ya mechi ya kwanza kufunga pia 5-1 na Guinea.
  Mchezo uliotangulia wa Kundi A leo, Cameroon nayo imejiweka mguu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Guinea katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Port Gentil, Gabon. 
  Kwa matokeo hayo, Guinea inafikisha pointi nne baada ya awali kushinda 5-1 dhidi ya wenyeji Gabon, wakati Cameroon inaokota pointi ya kwanza kutokana na sare hiyo, baada ya awali kufungwa 4-0 na Ghana.
  Mshambuliaji wa Les Syli Cadets, Djibril Fandje Toure aliifungia bao la kuongoza Guinea dakika ya 22 ambalo linakuwa bao lake la nne kwenye mashindano haya, kabla ya Stephane Zobo kuisawazishia Cameroon dakika ya 67.
  Mechi za Kundi B zinatarajiwa kuendelea kesho, Tanzania wakianza na Angola kabla ya Mali kupepetana na Niger. Ikumbukwe mechi za kwanza Jumatatu, Tanzania ilitoka sare ya 0-0 na Mali na Angola ilifungana 2-2 na Niger.
  Mchezaji wa Guinea,  Djibril Sylla (kushoto) akipambana na Ahmad Ngouyamsa Nounchili wa Cameroon
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GHANA YATINGA NUSU FAINALI, CAMEROON MGUU NJE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top