• HABARI MPYA

  Monday, May 15, 2017

  GABON, CAMEROON WAKIONA CHA MOTO UFUNGUZI AFCON U-17

  Na Mahmoud Zubeiry, LIBREVILLE
  WENYEJI Gabon wamekuwa na mwanzo mbaya kwenye Fainali za Vijana Afrika baada ya kufungwa mabao 5-1 na Guinea katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A Uwanja wa Port Gentil jana.
  Mabaoa ya Guinea yalifungwa na Djibril Toure dakika ya sita na 70, Nahodha Sekou Camara dakika ya 30, Elhadji Bah dakika ya 36 na Aguibou Camara dakika ya 45 wakati la Gabon la kufutia machozi lilifungwa na Fahd Moubeti aliyetokea benchi. 
  Mchezo mwingine wa Kundi A jana, mabingwa mara mbili, Ghana walianza vizuri kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Cameroon Uwanja wa Port Gentil, mabao ya Nahodha Eric Ayiah na kiungo Ibrahima Sulley kila mmoja mawili.
  Brou Abanga alifariki dunia Aprili 27, mwaka 2017, baada ya kupatwa na mshituko wa moyo wakati wa mazoezi na klabu yake, FC 105 mjini Libreville  

  Kabla ya mechi hizo wachezaji wa timu zote walisimama kimya pamoja na watu wote uwanjani kwa dakika moja kuomboleza msiba wa aliyekuwa kiungo wa Gabon, Moise Brou Abanga, aliyefariki dunia mwezi uliopita.
  Apanga alifariki Aprili 27, mwaka 2017, baada ya kupatwa na mshituko wa moyo wakati wa mazoezi na klabu yake, FC 105 mjini Libreville akiwa ana umri wa miaka 35 na mazishi yake yatafanyika mjini Libreville.
  Beki huyo wa kati pia, amewahi kuchezea Perugia na Brescia za Italia enzi zake na aliichezea Gabon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010 na 2012.
  Mechi za Kundi B zinachukua nafasi leo Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville kati ya Tanzania na Mali na Angola na Niger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GABON, CAMEROON WAKIONA CHA MOTO UFUNGUZI AFCON U-17 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top