• HABARI MPYA

  Sunday, May 14, 2017

  FAINALI ZA U-17 AFRIKA, KIPUTE CHAANZA LEO GABON

  Na Mwandishi Wetu, FRANCEVILLE 
  FAINALI za 12 za Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zinatarajiwa kuanza leo mjini Franceville, Gabon hadi Mei 28, mwaka huu itakapofikia tamati.
  Mechi mbili za Kundi A zinatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Franceville kuanzia Saa 10:00 jioni kati ya wenyeji Gabon dhidi ya Guinea na baadaye Saa 1:00 usiku kati ya Cameroon na Ghana.
  Mechi za Kundi B zitaanza kesho, kwa michezo miwili pia kuchezwa Uwanja wa Port-Gentil, ya kwanza Saa 9:00 Alasiri kati ya mabingwa watetezi, Mali na Tanzania wanaoshiriki kwa mara ya kwanza kabisa michuano hiyo na wa pili utazikutanisha Angola na Niger kuanzian Saa 12:00 jioni.
  Ghana watamenyana na Cameroon kuanzia Saa 1:00 usiku leo mjini Franceville

  Awali michuano hiyo ilikuwa ifanyike Madagascar kuanzia Aprili 2 hadi 16, mwaka huu lakini Kamati Kuu ya CAF chini ya rais wake wa zamani, Mcameroon Issa Hayatou ikaipokonya uenyeji nchi hiyo Januari mwaka huu kwa madai Kamati ya Ukaguzi iligundua mapungufu makubwa.
  Ingawa hiyo ilihusishwa na chuki za uchaguzi wa CAF, dhidi ya rais wa sasa, Ahmad ambaye ni Kiongozi wa soka ya Madagascar aliyejitosa kuwania Urais wa bodi ya Afrika.  
  Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia za U-17 zitakazofanyika nchini India Oktoba mwaka huu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FAINALI ZA U-17 AFRIKA, KIPUTE CHAANZA LEO GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top